MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 30 JUNI, 2019

                                                                        SIKU YA BWANA YA 2 BAADA YA UTATU

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

WITO WA KUINGIA UFALME WA MUNGU

 

 1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
 1. Wageni: Hakuna Mgeni aliyefika na cheti.
 1. Alhamisi ijayo tarehe 04/07/2019 saa 11.00jioni kutakuwa na kipindi cha maombi na maombezi. Karibu tupate akili na hekima ya kumjua Mungu. Usikose.
 1. Tunapenda kuwakaribisha wote katika vipindi vya kujifunza neno la Mungu siku za juma hapa Usharikani, Morning Glory inayoanza saa 12.00 – 1.00 asubuhi, siku ya Jumatatu hadi Ijumaa,  ambayo hukupa fursa ya kuanza kazi na uwepo wa Mungu.  Ibada ya Mchana kila siku saa 7.00 – 7.30 mchana ambayo inakupa nafasi ya kupata faragha  binafsi na Mungu.  Wote mnakaribishwa.
 2. Uongozi wa shule ya jumapili unapenda kuwataarifu wazazi kuwa ile siku ya kambi ya watoto iliyokuwa ifanyike jumanne iliyopita 25.06.2019 sasa itafanyika  kesho jumatatu 30.06.2019 Mkuza Kibaha. Hivyo watoto wataondoka hapa Kanisani saa 3.30 asubuhi kwa ajili ya kuanza safari ya kwenda Mkuza Kibaha.
 3. Tunaendelea na changizo juu ya kuendeleza Mradi wa ujenzi wa kituo cha Kiroho cha Kiharaka.  Washarika wote mnahimizwa kutoa na kukamilisha ahadi. Tarehe yetu ya kufunga hesabu hii ya changizo ni tarehe 31 Agosti 2019.  Karibuni tumfanyie Mungu sadaka.  Aidha Vitenge vya Kiharaka Vipo kwa bei ya sh. 10,000/=.
 4. Leo tarehe 30/06/2019 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika Karibuni.
 5. Mazoezi ya reformation yanaendelea kila siku ya jumanne saa 11.00 jioni. Tunaomba waimbaji wote muhudhurie kwa wingi ili kumrahisishia Mwalimu kufundisha kwa wakati.

 

 1. Tunategemea kupokea ugeni wa vijana kutoka Ujerumani tarehe  17/07/2019 na kuondoka tarehe 29/07/2019.  Uongozi wa umoja wa vijana unaomba wazazi na vijana kujitokeza kuwapokea na kuwatunza nyumbani mwetu kwa kipindi hiki cha siku 12 watakazokuwepo hapa Tanzania.  Kwa maelezo zaidi wasiliana na Mwenyekiti wa vijana Azania Front au Kamati ya Mahusiano

 

 1. Jumapili ijayo tarehe 07/07/2019 ni siku yetu ya maombi ya Usharika na ya kupokea Zaka toka mikononi mwa watoto wa Mungu.  Ni wakati wa kipekee wa kuja mbele za Mungu na sadaka zetu za fungu la kumi, na haja za mioyo yetu. Washarika tujiandae.

 

 1. Jumapili ijayo tarehe 07/07/2019 katika ibada ya kwanza Dada Annansia Godbless Uronu atamtolea Mungu shukrani ya pekee kumpa uhai wa kuishi mpaka leo, kumaliza masomo na kupata kazi pamoja na mambo makuu aliyomtendea katika maisha yake.
  1. Neno: Zaburi 121, Wimbo: Kwaya ya Agape

 

 1. NDOA

NDOA ZA WASHARIKA

Kwa mara ya Tatu tunatangaza ndoa za tarehe 06.07.2019

Ndoa hii itafungwa City Christian Centre kati ya

 

Bw. Luice Felix Matondo na   Bi. Irene Zacharia Nkya

 

Matangazo mengine ya ndoa yamebandikwa kwenye ubao matangazo karibu na duka letu la vitabu.

 1. Ibada za Nyumba kwa Nyumba
 • Wazo/Tegeta/Kunduchi/Bahari Beach/Ununio: …………………..
 • Mwenge/Kijitonyama/Makumbusho/Sinza/Ubungo/Makongo:Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo
 • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Kwa Dr. na Bibi Ruhago
 • Kinondoni: Watatangaziana

 

Zamu: Zamu za wazee leo ni kundi la Pili

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.