MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 30 APRILI, 2017

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI YESU KRISTO NI MCHUNGAJI MWEMA

 1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
 1. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na cheti.
 1. Kamati ya Misioni na Uinjilisti kwa niaba ya Uongozi wa Kanisa Kuu Azania Front, inapenda kuwatangazia watu wote kuwa leo ndio siku ya mwisho ya Semina ya NDOA NA FAMILIA iliyoanza jumamosi tarehe 22.04.2017. tunamshukuru sana Mungu kwa kutuwezesha kuwa na Semina hii na kumruhusu mtumishi wake Mch. Mathias Mushi na Mkewe Jessie Mushi kuihudumia semina hiyo kwa mafundisho, ushauri na maombi.  Tunawapongeza sana wote walioweza kufika ikiwa ni watoto, vijana, wajane, wagane na wanandoa. Tunajua mbegu iliyopandwa katika semina hii kwa wale waliolipokea neno itaota na kukua na kuzaa matunda yampendezayo Mungu.  Mungu awabariki sana.  Kipindi cha leo kitaanza saa 10.00.  Aidha siku ya alhamisi tarehe 04.05/2017 saa 11.30 jioni kutakuwa na kipindi cha maombi na maombezi.  Wote mnakaribishwa.
 1. Ukarabati wa vioo vya madirisha ya Kanisa kuu ambao ulifadhiliwa kwa kiasi furani na ubalozi wa ujerumani hapa Dar es Salaam umekamilika. Na sasa vioo vyetu vimekaa vizuri kama mnavyoona vinapendeza.
 1. NDOA

NDOA ZA WASHARIKA

Kwa mara ya Kwanza tunatangaza ndoa  za tarehe 13/05/2017

SAA 8.00 MCHANA

Bw. Salim Athuman Kisuda   na     Bi. Sarah Laili Mussa

SAA 10.00 JIONI

Bw. Nzota Gideon Killango    na     Bi. Margareth Frank Mtui

 

Kwa mara ya Pili tunatangaza ndoa  za tarehe 13/05/2017

SAA 9.00 ALASIRI

Bw. Erick Godian Mwakipesile        na     Bi. Adeline Josephine Mmbaga

SAA 10.00 JIONI

Bw. Ajelandro Mushobozi Sindano na     Bi. Rehema Mahmoud Kikwere

Kwa mara ya Tatu tunatangaza ndoa  za tarehe 06/05/2017

SAA 6.00 MCHANA

Bw. Morries Walter Shangali          na     Bi. Elke Norah Sumari

 

SAA 10.00 JIONI

Bw. Eliah Emmanuel Kinyunyu      na     Bi. Emilia Bonifas Mdamba

              

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

 1. Ibada za Nyumba kwa Nyumba
 • Upanga: Kwa Bwana na Bibi Ndosi
 • Kinondoni:  Kwa Prof. na Bibi Kulaba
 • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Watatangaziana
 • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Watatangaziana
 • Oysterbay/Masaki: Watatangaziana
 • Tabata: Watatangaziana
 • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Mama Ruth Korosso
 • Mjini kati: Kwa Bwana na Bibi Stanley Mkocha
 • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Kwa Dk na Bibi Kinasha