MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 29 APRILI, 2018

SOMO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI KILA MWENYE PUMZI NA AMSIFU BWANA

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni:  Hakuna wageni waliotufikia na cheti.

3. Alhamisi ijayo tarehe 03/05/2018 kutakuwa na kipindi cha maombi na maombezi hapa Usharikani kuanzia saa 11.30 jioni.  Fursa hii ambayo wengi wamepata majibu ya haja zao imetayarishwa kwa ajili yako, usikose.  Wote mnakaribishwa.

4. Vitabu vipya vya Tumwabudu Mungu wetu vipo tayari.  Vitauzwa hapo nje kwa bei ya Sh. 12,000/= tu.  Pia vitenge vya Kiharaka vipo kwa bei ya Sh. 10,000/= tu.

5.Jumapili ijayo tarehe 06/05/2018 Familia ya Bwana na Bibi Itemba itamtolea Mungu shukrani kwa kuwatunza kipindi chote tangu mama yao mpendwa alipotwaliwa na Bwana mwaka mmoja uliopita. Neno: Zab. 23

6. NDOA.

Matangazo ya ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

7. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

- Upanga: Kwa A. Tabay

- Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Jackson Kaale

- Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Kwa Bwana na Bibi Kowero

- Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Eng. na Bibi Zebadiah Moshi

- Oysterbay/Masaki: Kwa Mama Ruth Chipeta

- Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Matei.

                                            

Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Pili.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.