MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 26 MACHI, 2017

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI YESU NI CHAKULA CHA UZIMA

 1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
 1. Wageni:  wageni waliotufikia na cheti ni:- Mrs Particia Namonje Sinyinza toka United Church of Zambia – St. Peters Mwenzo.
 2. Leo hatutakuwa na kipindi cha maombi na maombezi hadi siku ya alhamisi  tarehe 30.03.2017 ambacho kitaongozwa na Mwinjilist Jacob Mlawi.  Yesu ataendelea kujidhihirisha kwa mkono wenye nguvu na mamlaka katika Roho Mtakatifu. Wote mnakaribishwa.
 1. Jumatano ijayo tarehe 29/03/2017 saa 11.00 jioni kutakuwa na ibada kama kawaida ya Kwaresma.  Zamu za wazee itakuwa ni kundi la Kwanza.
 1. Leo tutashiriki chakula cha Bwana.  Washarika karibuni
 1. Kamati ya Uhusiano na habari, inawatangazia wale wote waliojiandikisha kwa safari ya Messiah Marekani ya Mwezi Octoba, wafike ofisini kwa Katibu wa Usharika na kujaza fomu maalum ya taarifa zao ndani ya wiki hii ili kuwezesha taratibu nyingine kuendelea.
 2. TANZIA

Usharika unasikitika kutangaza kifo cha msharika na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Mama Apaisaria Kilewo. Ibada ya kumuaga itafanyika leo saa 8.00 mchana hapa Usharikani.  Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana libarikiwe.

 1. Ibada za Nyumba kwa Nyumba
 • Upanga: Kwa Bwana na Bibi Mbwilo
 • Kinondoni:  Kwa Bwana na Bibi Jackson Kaale
 • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: watashiriki ibada hapa usharikani
 • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Watangaziana
 • Oysterbay/Masaki: watashiriki ibada hapa usharikani
 • Tabata: Watangaziana
 • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Sangiwa
 • Mjini kati: Watangaziana
 • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Watangaziana