MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 22 OKTOBA, 2017

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI IMANI ILETAYO USHINDI

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna Mgeni aliyetufikia na cheti.

3. Kipindi cha maombi na maombezi kitakuwepo leo kuanzia saa 9.00 alasiri. Aidha Alhamisi ijayo tarehe 26/10/2017 kutakuwa na maombi na maombezi kuanzia saa 11.00 jioni. Wote mnakaribishwa.

4. Tunapenda kuwatangazia wazazi wanaobariki watoto tarehe 26/12/2017 kuwa watoto watavaa Tshirt, Sketi nyeusi na viatu vyeupe. Wavulana watavaa Tshirt, suruali nyeusi na viatu vyeusi. Tunawaomba wazazi  mpeleke mapema Sh. 15,000/= kwa Parish Worker. Ibada hiyo itafanyika hapa Usharikani kuanzia saa 2.00 asubuhi.

5. Tunapenda kuwatangazia washarika kuwa Sikukuu ya Mavuno mwaka huu itafanyika tarehe 12/11/2017 katika ibada zote mbili kama kawaida.  Ibada ya pili siku hiyo itaanza saa 4.00 asubuhi.  Washarika tuikumbuke siku hiyo kwa maombi.  Mungu awabariki.

6. Kikao cha Vicoba ya Wajane na Wagane wa Azania Front kitafanyika jumamosi ya tarehe 28 Oktoba saa 3.00 asubuhi.  Wajumbe wote wanaohusika wanakaribishwa kuhudhuria kikao hicho.

7. Jumapili ijayo tarehe  29/10/2017 katika ibada ya pili saa tatu na nusu asubuhi familia mbili zitamtolea Mungu shukrani.

a) Familia ya Brigedia Generali Mstaafu Potiphar Sande Ligate na Mama Elizabeth Ligate watamshukuru Mungu kwa mambo mengi aliyowatendea ikiwa ni pamoja na kutimiza miaka 50 ya ndoa yao.

                                            Neno: Warumi 8:28

                                            Wimbo: Kwaya Kuu (Mungu kanilinda mimi), TMB 132

 

b) Familia ya Mama Mrema na Familia ya Goodluck Mrema  nao pia watamshukuru kwa mambo mengi aliyowatendea ikiwa ni pamoja na Goodluck Mrema kufikisha miaka 5 ya ndoa.

                                            Neno: Zaburi 23; Zaburi 121.

                                            Wimbo: Kwaya Kuu (Yesu Mwokozi yu mlinzi wangu)

 

8. NDOA

NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 04/11/2017 NDOA HII ITAFUNGWA PAROKIA YA TABATA

Bw. Eddy Salum Kiluvya             na       Bi. Awaremi  Noe Kimaro

TAREHE 03/11/2017

SAA 8.00 MCHANA

Bw. Miguel Emmanuel Kilwanda na       Bi. Angela Kitumbo Janas

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 28/10/2017

SAA 9.00 ALASIRI

Bw. Frank Godfrey Kanza           na       Bi. Eva Wynjones Kanumba

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

 

9. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

 

a) Upanga: Watatangaziana

b) Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Edward Mkony

c) Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Watatangaziana

d) Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Askofu na Mama Alex Malasusa

e) Oysterbay/Masaki: Kwa Bibi Joyce Kasyanju

f) Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo:  Watatangaziana Mjini kati: Kwa Bwana na Bibi Kabezi

g) Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Kwa Bwana na Bibi Mcharo Mlaki

 

Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Kwanza.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.