MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 02 APRILI, 2017

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI YESU NI MPATANISHI

 1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
 1. Wageni:  wageni waliotufikia na cheti ni
 • Issa Aroni Mwaigomole toka usharika wa Songwe viwandani Dayosisi ya Konde Mbeya.
 • Margaret Sipendi toka Mtaa wa Msimbazi Tabata Dayosisi ya Mashariki na Pwani – anahamia hapa Azania Front
 1. Leo jioni saa kumi kutakuwa na kipindi cha maombi na maombezi ambacho kitaongozwa na Mwinjilist Jackon Mndeme kutoka KKKT Kijitonyama aidha siku ya alhamisi tarehe 06/04/2017 pia kutakuwa na kipindi cha maombi na maombezi kitakachoongozwa na Mwinjilisti Jacob Mlawi kutoka KKKT Mbezi Lous.
 1. Uongozi wa Umoja wa Wanawake unapenda kuwakumbusha wanawake kuwa tamasha la uimbaji ni tarehe 13.05.2017 mazoezi yameanza. Tunaomba wanawake wa Kwaya Kuu, Kwaya ya Upendo, Vijana, Agape na tarumbeta waungane na kwaya ya wanawake ili kufanikisha siku hiyo ya Tamasha.
 1. Uongozi wa shule ya jumapili unapenda kuwaomba wazazi kuwaleta watoto kila siku ya jumamosi saa 9.00 alasiri ili waanze mazoezi ya nyimbo kwa ajili ya tamasha lao. Mungu awabariki.
 1. Kamati ya Misioni na Uinjilisti kwa niaba ya uongozi wa Usharika unapenda kuwatangazia washarika kuwa kuanzia tarehe 23/04/2017 hadi tarehe 30/04/2017 kutakuwa na semina ya ndoa itakayofundishwa na Mchungaji Mathias Mushi toka KKKT Arusha. Ratiba kamili kuhusu semina hiyo itatangazwa hapo baadaye. Washarika mnaombwa kuiombea semina hii.  Wote mnakaribishwa.
 1. Jumatano ijayo tarehe 05/04/2017 saa 11.00 jioni kutakuwa na ibada kama kawaida ya Kwaresma.  Zamu za wazee itakuwa ni kundi la Pili.
 1. Leo tutamtolea Mungu fungu la kumi.

 

 1. Ibada za Nyumba kwa Nyumba
 • Upanga: Kwa Bw na Bibi Mduma
 • Kinondoni:  Kwa Bwana na Bibi Elinafika Mkumbwa
 • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: watashiriki ibada hapa usharikani
 • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi Zebadia Moshi. Ibada itafanyika ijumaa saa 10 jioni
 • Oysterbay/Masaki: watashiriki ibada hapa usharikani
 • Tabata: Watangaziana
 • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Sangiwa
 • Mjini kati: kwa mama Victoria mwansasu
 • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Kwa Bwana na Bibi Frank Korassa