MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 19 FEBRUARI, 2017

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI NENO LA MUNGU LINA NGUVU

  1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

  1. Wageni:  Hakuna wageni waliotufikia na cheti .
  1. Kamati ya Misioni na Uinjilisti inapenda kuwatangazia kuwa kikundi chetu cha Maombi na Maombezi kitaendelea siku ya Alhamisi tarehe 23/02/2017 saa 11.30 jioni.  Njooni wote wenye mizigo na mnaotaka kutoka katika vifungo vya shetani, na wagonjwa watapata huduma ya maombi.  Mnenaji atakuwa Mwinjilisti Jacob Mlawi. Aidha Kamati ya Misioni na Uinjilisti inawaarifu vikundi vyote hapa Usharikani kuwa kutakuwa na kikao cha viongozi siku ya Jumanne tarehe 21/02/2017 saa 11.00 jioni hapa hapa Usharikani.  Kila Kikundi kiwakilishwe na Mwenyekiti na Katibu.  Kikao kitahusu kujipanga kwa ajili ya Kwaresma, Pasaka na Kantate Domino.  Pia wajumbe wa Kamati ya Kinanda wanatangaziwa kuwa kutakuwa na kikao cha Kamati siku ya Jumatano saa 11.00 jioni hapa Usharikani.
  1. Uongozi wa Wanawake unapenda kuwajulisha wanawake wote kuwa mwezi wa tatu kutakuwa na majukumu yafuatayo:
  • Tarehe 03/03/2017 ni siku ya maombi ya dunia yatakayofanyika katika Kanisa la jeshi la wokovu kwenye viwanja vya sabasaba.  Sare ni vitenge vya mbaombi ya dunia.
  • Tarehe 05.03.2017 ni siku ya Wanawake kuongoza ibada. Sare ni vitenge vya KKKT.
  • Tarehe 08/03/2017 ni siku ya Wanawake kurudia maombi hapa usharikani.
  • Wanawake wote mnaombwa kukutana hapa Usharikani tarehe 25.02.2017 saa 4.00 asubuhi kwa ajili ya maandalizi ya kuhudumu kwenye maombi. Viongozi watagawa fomu za kujaza hivyo tunaomba kila mwanamke aweke kile anachopenda kufanya siku hiyo
  1. Jumapili ijayo tarehe 26/02/2017 tutashiriki Chakula cha Bwana.  Washarika tujiandae
  1. Uongozi wa shule ya jumapili unapenda kuwakumbusha washarika kuwa jumapili ijayo tarehe 26.02.2017 ni siku ya maombi ya dunia kwa watoto wa shule ya jumapili, hivyo sadaka yao ya siku hiyo watapekeka Mtoni kwa watoto wenye utindio wa Ubongo tarehe 04.03.2017.   Kama kuna mtu mwenye chochote iwe ni nguo, sabuni, mafuta ya kupaka, fedha walete ofisi za usharika ili watoto waweze kwenda navyo siku hiyo. Mungu awabariki.
  1. NDOA:

Kwa mara tatu tunatangaza ndoa za tarehe 25/02/2017

Bw. Efraim Simon Mwaipungu       na     Bi. Doris Jamesy Ambangile

Matangazo mengine yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu

 

  1. Ibada za Nyumba kwa Nyumba
  • Upanga: Watangaziana
  • Kinondoni:  Kwa Mama Tabu Ndziku
  • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Kwa Bwana na Bibi Itemba
  • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Watangaziana
  • Oysterbay/Masaki: Watangaziana
  • Tabata: Watangaziana
  • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Mzee Evatt Kuzilwa
  • Mjini kati: Kwa Elisifa Ngowi
  • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio:  Kwa David Korosso

Zamu: Zamu za wazee leo ni kundi la Pili.

 

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.