MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 18 FEBRUARI, 2018

SOMO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI TUKIMTEGEMEA MUNGU TUTASHINDA MAJARIBU

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.

3. Jumatano ijayo tarehe 21/02/2018 tunaendelea na ibada ya Kwaresma kama kawaida. Washarika wote mnahimizwa kuiadhimisha. Tunaendelea na mafundisho maalumu juu ya "UWEZA NA NGUVU YA DAMU YA YESU". Mnenaji atakuwa ni Mr. Charles Macha kutoka Mtoni Kijichi KKKT. Mafundisho yatakuwa ni  siku tatu Jumatano, Alhamis na Ijumaa kuanzia saa 11.00 jioni. Jumuiya zetu zitaongoza liturgia ya ibada za Kwaresma siku ya Jumatano kwa kupokezana. Hivyo hakutakuwa na vipindi vya Maombi na Maombezi siku za Alhamis kwa kipindi cha Kwaresma, kwani  mafundisho maalum yataendelea.

4. Jumapili ijayo tarehe 25/02/2018 tutashiriki chakula cha Bwana. Kama Kawaida siku ya Kushiriki ibada ya pili itaanza saa 4.00 asubuhi. Washarika tujiandae.

5. Jumamosi ijayo tarehe 24/02/2018 saa 3.00 asubuhi kutakuwa na mkutano wa Wajane na Wagane wa Azania Front.  Wahusika wote wanaombwa kuhudhuria mkutano huo.

6. Washarika wanataarifiwa kuwa tunaanza matayarisho ya igizo la Pasaka. Wale wote wanaosikia wito wa kuhubiri kupitia igizo hili wakutane na Mwenyekiti wa Misioni na Uinjilisti.

7. Jumapili ijayo tarehe 25/02/2018 katika ibada ya pili familia ya Bwana na Bibi Andrew Makange watamshukuru Mungu kwa kufanikisha ndoa yao iliyofungwa tarehe 30/12/2017 hapa  Usharikani.

Neno: Zaburi 23.  Wimbo: TMB. 196

8. Tunapenda kuwatangazia washarika kuwa yeyote ambaye hakujaza fomu kwa ajili ya namba mpya za bahasha asitumie bahasha yeke aliyokuwa anatumia zamani afike ofisini ili kupata namba mpya.  Kuna baadhi ya Washarika wanatumia namba zao za zamani na kusababisha usumbufu  kwa wengine.

9. Jumapili ijayo tarehe 25/02/2018 Kwaya ya Wanawake itahudumu Mtaa Chole/Kwale. Washarika tuwaombee.

 

10. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

  - Upanga: Watashiriki semina hapa usharikani

  - Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Watashiriki semina hapa usharikani

  - Oysterbay/Masaki: Watashiriki ibada hapa usharikani Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa ……….

  - Mjini kati:  Kwa Bwana na Bibi Elisifa Ngowi

  - Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio:Kwa Bwana na Bibi Mcharo Mlaki

 

Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Pili.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.  

 

                                                                               RATIBA YA HUDUMA KATIKA

IBADA ZA JUMATANO KIPINDI

CHA KWARESMA

 

 

TAREHE

 

 

 

JUMUIYA

 

KWAYA INAYOONGOZA

 

 

MTUMISHI

21/02/2018

 

UPANGA  NA  MJINI KATI,

 

KWAYA KUU

 

KWAYA YA VIJANA

 

 

 

 

28/02/2018

 

ILALA/CHANG’OMBE/MIVINJENI,

NA

KINONDONI

 

KWAYA YA UPENDO,

 

KWAYA YA AGAPE

 

 

07/03/2018

 

WANAWAKE

 

KWAYA YA KINAMAMA,

 

TARUMBETA

 

 

14/03/2018

 

KAWE/MIKOCHENI/MBEZI BEACH

 

KWAYA KUU,

 

KWAYA YA VIJANA

 

 

 

21/03/2018

 

OYSTERBAY/MASAKI

NA

KIJITONYAMA/SINZA/MWENGE/

MAKUMBUSHO/UBUNGO

KWAYA YA KINAMAMA,

 

TARUMBETA

 

 

28/03/2018

 

TABATA

NA

WAZO/TEGETA/KUNDUCHI/

BAHARI BEACH/UNUNIO

 

 

KWAYA YA UPENDO

 

KWAYA YA AGAPE

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Viongozi wa vikundi na Jumuiya husika wasimamie utekelezaji wa ratiba hii.