MATANGAZO YA USHARIKA

 TAREHE 17 JUNI, 2018

SOMO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI TUDHAMIRIE MAMOJA

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni:  Hakuna wageni waliotufikia na cheti

3. Tunamshukuru Mungu kwa jinsi anavyojidhihirisha tunapokutana kwa masomo, maombi na maombezi siku za alhamisi jioni.  Alhamisi ijayo tarehe 21/06/2018 kutakuwa na kipindi cha maombi na maombezi yatakayoanza saa 11.30 jioni. Wote mnakaribishwa.

4. Jumapili ijayo tarehe 24/06/2017 tutashiriki Chakula Cha Bwana.  Hivyo ibada ya pili itaanza saa 4.00 asubuhi.  Washarika tujiandae.

5. Mkutano wa VICOBA ya Wajane na Wagane utafanyika jumamosi ya tarehe 30/06/2018 saa 3.00 asubuhi. Wahusika wote wanaombwa kuhudhuria.

6. NDOA.

NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 05/07/2018

 

SAA 08.00 MCHANA

Bw. Kiiza Emanzi Kemanzi     na     Bi Joyce Dennis Kasyoba

 

TAREHE  07/07/2018   

SAA 05.00 ASUBUHI

  • Bw. Emmanuel Tumsifu Jonas naBi Jacqueline Benezeth Benjamin

 

SAA 08.00 MCHANA

  • Bw. Hans Ikamba Lasway naBi. Ikumbo Charles  Nyange

 

SAA 10.00 JIONI

  • Bw. Christopher Michael Laban na Bi VeronicaJosephat Kweka

 

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 30/06/2018

SAA 9.00 ALASIRI

Bw. John Ndisha Furahini   na        Bi Anneth Adolph Makenja

 

NDOA HII IFUATAYO ITAFUNGWA KANISA LA KATOLIKI PAROKIA YA UPANGA.

Bw. Derick Mujuni Kajukano   na   Bi. Anita Abednego Kinasha

 

Matangazo mengine ya ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

 

7. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

  • Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi T.M. Onesmo
  • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Kwa Dk na Bibi David Ruhago
  • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Mama Happines Chamungwana
  • Mjini kati:  Kwa Bwana na Bibi Kabezi
  • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Simon Jengo
  • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Kwa ………
  • Tabata: Kwa Oscar na Imaculate

                                              

8. Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Kwanza.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.