MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 15 JANUARI, 2017

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI MUNGU HUBARIKI NYUMBA ZETU

 1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
 1. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na cheti:

     2a.    Ibada ya Maombi na maombezi leo haitakuwepo ila itaanza tena 19/01/2017. Na siku hiyo itakuwa ni ibada ya shukrani kwa kupata nafasi ya                kuanza  tena huduma hii mwaka 2017. Mnenaji atakuwa ni Mtumishi Sweetbert Lugemalila.

 1. Kwaya ya Usharika (Kwaya Kuu) inategemea kusafiri ijumaa ijayo tarehe 20/01/2017 mpaka tarehe 22/01/2017  usharika wa Nkwarungo Moshi. Katika ziara hiyo watatembelea hospitali ya Nkwarungo. Hivyo kama kuna msharika angependa kuungana nao kwa vitu au fedha kwa ajili ya wagonjwa wanakaribishwa ofisi ya usharika. Washarika tuwaombee.
 1. Usharika umepata mwaliko wa kutembelea Usharika rafiki wa Messiah ulioko Marguette Michigan Marekani mwezi wa Oktoba mwaka huu.  Ujumbe utakuwa na watu 10, nusu wanawake na nusu wanaume.  Wenyeji watahusika na malazi, chakula na usafiri.  Washarika watagharamia usafiri wao wenyewe kiasi cha USD 2000 kwa tiketi ya ndege kwenda na kurudi, na USD 200 hadi 500 kwa matumizi binafsi.  Watakaopenda kujiunga kwenye ziara hii, wajiandikishe ofisini kwa Katibu wa Chaplain mapema.  Taarifa  muafaka zitaendelea kutolewa jinsi mipango inavyosonga mbele.
 1. Uongozi wa Umoja wa wanawake unaendelea kuwashukuru sana washarika waliojitoa kuchangia ada watoto yatima katika kituo cha Watoto wetu Tanzania Donbosco aidha wanawakumbusha wale walio ahidi watimize ahadi zao pia ambao wangependa kuchangia wanakaribishwa. Mungu awabariki sana.
 1. Ibada za Nyumba kwa Nyumba
 • Upanga: Watatangaziana
 • Kinondoni:  Watatangaziana
 • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Watatangaziana
 • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Bwana na Bibi Alex Lema
 • Oysterbay/Masaki: Watatangaziana
 • Tabata: Watatangaziana
 • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Bwana na Bibi S. Jengo
 • Mjini kati: Kwa Bwana na Bibi Kabezi
 • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio:  Watatangaziana