MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 12 AGOSTI, 2018

SOMO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI MUNGU HUWAINUA WANYENYEKEVU

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na cheti.

3. Tumekuwa na kipindi kizuri sana siku ya Alhamisi tarehe 09 Agosti, 2018 na wengi walifunguka.Kwa hiyo Alhamisi ijayo tarehe 16/08/2018 tutakuwa na kipindi kingine saa 11.30 jioni.Washarika wote mnakaribishwa.Aidha leo jumapili saa 10.00 jioni hapa usharikani tutakuwa na kipindi maalum cha maombi na maombezi kwa ajili ya watoto na vijana wetu.Njoo na watoto, vijana wako, picha yake au jina, tumlilie Mungu juu ya yao.Neno Kuu ni Isaya 42:22-23.Usiache kuja, mwalike na jirani, bila kujali imani yao.Wote mnakaribishwa.

4. Mkutano wa Vicoba ya Wajane na Wagane wa Azania Front utafanyika jumamosi ya tarehe 25/08/2018 saa 3.00 asubuhi. Wahusika wote wanaombwa kuhudhuria mkutano huo.

5. Umoja wa Wanawake Azania wanawashukuru wanawake wote waliohudhuria Semina ya Wanawake siku ya Jumatano tarehe 08/08/2018.Pia wanawakumbusha washarika juu ya kuchangia ukuta wa shule yetu ya Mkuza.Uongozi unashukuru kwa kila mmoja anayejitoa kwa kuchangia. Mungu awabariki

6. Jumapili ijayo tarehe 19/07/2018 katika ibada ya pili saa 3.30 asubuhi familia ya Bwana na Bibi George Israel Mnyitafu watamshukuru Mungu kwa mambo mengi aliyowatendea ikiwa ni pamoja na mtoto wao kumaliza kidato cha sita na kufanya vizuri na kupata chuo kuendelea na masomo.

Neno: Mithali 4:10-18,  Wimbo: Kwaya Kuu (Yesu nitakuimbia kwa wingi wa rehema zako)

 

7. NDOA ZA WASHARIKA

    KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 01 NA 02/09/2018

 

   01/09/2018

   SAA 09.00 ALASIRI

Bw. Paulo Carlos Chalamila         na     Bi Anety Mathew Kagaruki

   02/09/2018

   SAA 08.00 MCHANA

Bw. Isaria K. Kilewo         na     Bi Lilian J. Mella

 

Matangazo mengine ya ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu

 

8.  Ibada za Nyumba kwa Nyumba

    - Upanga: Kwa Bwana na Bibi Happness Nkya

    - Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi T.M Onesmo

    - Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Kwa Bwana na Bibi Itemba

    - Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi Freeman Mbowe

    - Oysterbay/Masaki: Watatangaziana

    - Mjini kati:  Kwa Bwana na Bibi Stanley Mkocha

    - Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo:Kwa Bwana na Dr. Matee

    - Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Kwa Bwaa na Bibi Lawence Mlaki

    - Tabata: Kwa Mama Urio

   

Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Kwanza.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.