MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 11 MARCH, 2018
SOMO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI TUTUNZE UUMBAJI
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.
3. Uongozi wa Usharika unapenda kuwatangazia washarika wote kwamba Jumapili ijayo tarehe 18/03/2018 tutakuwa na ibada ya maombi kwa Usharika mzima katika ibada zote mbili. Kwa jinsi hii washarika wanataarifiwa kuandaa mahitaji yao na kuyaandika ili kuwasilishwa madhabahuni siku hiyo. Tutakuwa na sadaka maalumu ya kusindikiza maombi hayo. Siku hiyo ibada ya pili itaanza saa 4.00 asubuhi. Washarika wote tuiombee siku hiyo.
4. Jumatano ijayo tarehe 14/03/2018 tunaendelea na ibada ya Kwaresma kama kawaida. Washarika wote mnahimizwa kuiadhimisha. Tunaendelea na mafundisho maalumu juu ya "MAMLAKA UWEZA NA NGUVU YA DAMU YA YESU". Mafundisho yatakuwa ni siku tatu kama kawaida Jumatano, Alhamis na Ijumaa kuanzia saa 11.00 jioni. Jumuia ya KAWE/MIKOCHENI/MBEZI BEACH itaongoza liturgia ya ibada ya Kwaresma siku ya Jumatano, Kwaya zitakazohudumu ni Kwaya Kuu na Kwaya ya Vijana. Aidha Maombi na Maombezi siku za Alhamisi yataendelea kwa kipindi cha Kwaresma, yakiambatana na mafundisho maalum.
5.Tunapenda kuwatangazia washarika kuwa yeyote ambaye hakujaza fomu kwa ajili ya namba mpya za bahasha asitumie bahasha yeke aliyokuwa anatumia zamani afike ofisini ili kupata namba mpya. Kuna baadhi ya Washarika wanatumia namba zao za zamani na kusababisha usumbufu kwa wengine.
6. Uongozi wa Usharika unapenda kuwatangazia washarika wote kwamba tarehe 24/03/2018 saa 4.00 asubuhi tutakuwa na ibada maalum itakayoambatana na Chakula cha Bwana kwa washarika wetu wote wenye umri kuanzia miaka 65 na kuendelea. Pia kutakuwa na maongezi ya pamoja. Wazee wote hao wanakaribishwa. Tungependa kupata muitikio wa idadi ya watakaoshiriki katika ibada hii. Kwa Wazee ambao watahitaji huduma ya usafiri tunaomba taarifa zao kwenye ofisi ya Chaplain.
7. Jumapili ijayo tarehe 18/03/2018 Sister Elipendo Mkandawire na familia yake watatoa shukrani ya pekee kwa mambo mengi Makuu Mungu aliyomtendea. Ikiwa ni pamoja na kutimiza miaka 70 mwezi huu, kufanya kazi ya Muuguzi/Mkunga kwa miaka 50 bila tatizo lolote tangu mwaka 1967 mpaka Desemba 2016.
Neno: Zaburi 105:1-4, Wimbo: 312 Ubeti wa 1 na wa 5.
8. Ibada za Nyumba kwa Nyumba
- Upanga: Watashiriki semina hapa usharikani
- Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Alpha Mlenga.
- Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Watashiriki semina hapa usharikani
- Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Watashiriki semina hapa usharikani
- Oysterbay/Masaki: Watashiriki ibada hapa usharikani Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Mzee Evatt Kuzilwa.
- Mjini kati: Kwa Bibi Twilumba Talawa
- Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio:Kwa Dr na Bibi Nangawe
- Tabata: Kwa ……………………………
Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Kwanza.
Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.
RATIBA YA HUDUMA KATIKA
IBADA ZA JUMATANO KIPINDI
CHA KWARESMA
TAREHE |
|
JUMUIYA |
KWAYA INAYOONGOZA
|
MTUMISHI |
21/02/2018 |
|
UPANGA NA MJINI KATI,
|
KWAYA KUU
KWAYA YA VIJANA
|
|
28/02/2018 |
|
ILALA/CHANG’OMBE/MIVINJENI, NA KINONDONI
|
KWAYA YA UPENDO,
KWAYA YA AGAPE
|
|
07/03/2018 |
|
WANAWAKE
|
KWAYA YA KINAMAMA,
TARUMBETA
|
|
14/03/2018 |
|
KAWE/MIKOCHENI/MBEZI BEACH
|
KWAYA KUU,
KWAYA YA VIJANA
|
|
21/03/2018 |
|
OYSTERBAY/MASAKI NA KIJITONYAMA/SINZA/MWENGE/ MAKUMBUSHO/UBUNGO |
KWAYA YA KINAMAMA,
TARUMBETA
|
|
28/03/2018 |
|
TABATA NA WAZO/TEGETA/KUNDUCHI/ BAHARI BEACH/UNUNIO
|
KWAYA YA UPENDO
KWAYA YA AGAPE
|
|
|
|
|
|
|
Viongozi wa vikundi na Jumuiya husika wasimamie utekelezaji wa ratiba hii.