Date: 
14-09-2021
Reading: 
Marko 1:35-39

Jumanne asubuhi;

14.09.2021

Marko 1:35-39

[35]Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko.

[36]Simoni na wenziwe wakamfuata;

[37]nao walipomwona wakamwambia, Watu wote wanakutafuta.

[38]Akawaambia, Twendeni mahali pengine, mpaka vijiji vilivyo karibu, nipate kuhubiri huko nako; maana kwa hiyo nalitokea.

[39]Akaenda akihubiri katika masinagogi yao, katika nchi yote ya Galilaya, na kutoa pepo.

Mungu hujishughulisha na mambo yetu;

Baada ya sala ya asubuhi, Yesu anafuatwa na wanafunzi wake wakimwambia kuwa watu wanamtafuta. Yesu siyo tu kwamba yuko tayari kuwapokea hao watu waliomtafuta, bali alikuwa tayari kwenda pengine pote kuhubiri, akisema ndiyo maana alikuja.

 

Ujumbe huu asubuhi hii unatukumbusha kuwa Yesu yuko tayari kutupokea sote, wakati wote. Ndiyo maana alikuja. Wajibu wetu ni kumtafuta kwa bidii. Tunamtafutaje? Kwa kusoma na kulitii neno lake, tukimpa maisha yetu ayatawale, kama Mwokozi na Mpatanishi wetu.

 

Tukiishi ahadi ya ubatizo wetu, na kuikaribia meza yake kwa haki, tunajihakikishia kuwa kwake, naye hutupokea, maana hujishughulisha na mambo yetu. Siku njema.

Heri Buberwa