Date: 
28-09-2022
Reading: 
Marko 12:28-34

 Jumatano asubuhi tarehe 28.09.2022

Marko 12:28-34

[28]

Na mmojawapo wa waandishi akafika, akawasikia wakisemezana naye, akatambua ya kuwa amewajibu vema, akamwuliza, Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza?

[29]Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja;

[30]nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.

[31]Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.

[32]Yule mwandishi akamwambia, Hakika, Mwalimu, umesema vema ya kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye;

[33]na kumpenda yeye kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama nafsi yako, kwafaa kuliko sadaka nzima za kuteketezwa na dhahibu zote pia.

[34]Naye Yesu, alipoona kwamba amejibu kwa busara, alimwambia, Wewe hu mbali na ufalme wa Mungu. Wala hakuthubutu mtu kumsaili neno tena tokea hapo.

Uchaguzi wa busara;

Mwandishi mmoja alimuuliza Yesu kuhusu amri. Yesu akampa amri kuu. Ya kwanza kumpenda Mungu, na ya pili kumpenda jirani. Mwandishi inaonekana alielewa, maana anaonekana akiongezea kuwa Mungu ni mmoja astahiliye kuabudiwa. Mwandishi anaongeza kuwa kumpenda Mungu kwafaa kuliko sadaka za kuteketezwa. 

Amri za Mungu tunazifahamu. Huwa zinahusu Watu na Mungu (amri 4 za kwanza) zilizobaki zinahusu watu na watu. Yesu alifupisha na kuweka amri kuu, ya kwanza kumpenda Mungu na ya pili kumpenda jirani. Kutimiza amri kuu ni kutimiza amri zote. Tuchague kutimiza amri za Mungu kwa kumpenda Mungu na jirani zetu.

Jumatano njema