Date: 
30-07-2021
Reading: 
Maombolezo 3:25-26

IJUMAA TAREHE 30JULAI 2021, ASUBUHI

Maombolezo 3:25-26

25 Bwana ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwa hiyo nafsi imtafutayo.
26 Ni vema mtu autarajie wokovu wa Bwana Na kumngojea kwa utulivu.

Wema wa Mungu watuvuta tupate kutubu;

Yeremia baada ya kupitia shida na mateso, akipoteza mali na watoto, anaomboleza akionesha kuwa Upendo wa Mungu huvumilia. Leo asubuhi tunasoma kuwa Bwana ni mwema kwa wote wamtafutao, akiwasihi waungoje wokovu wa  Bwana na kumngojea kwa utulivu. Katika kungojea huko, Bwana hutuvumilia, ndio maana hutupa nafasi ya kutubu. Unaitumiaje nafasi hiyo?

Kumngojea kwa utulivu ni kuishi kwa msingi wa neno la Mungu, tukijua wokovu upo kwa ajili yetu.  Hatuwezi kuupata huo wokovu bila kutubu dhambi. Tukitubu dhambi tunayo hakika ya wokovu.

Ijumaa njema


FRIDAY 30TH JULY 2021

LAMENTATIONS 3:25-26 (NIV)


25 The Lord is good to those whose hope is in him,
    to the one who seeks him;
26 it is good to wait quietly
    for the salvation of the Lord.

Read full chapter

God's goodness draws us to repentance;

Jeremiah, after going through hardships and suffering, losing property and children, mourns to show that God's love endures. This morning we read that the Lord is good to all who seek Him, urging them to wait for the Lord's salvation and to wait patiently for Him. In the meantime, the Lord is patient with us, which is why He gives us the opportunity to repent. How do you take advantage of that opportunity?

Waiting for Him patiently, is to live on the basis of God's word, knowing that salvation is for us. We cannot attain that salvation without repenting of sin. If we repent of our sins we are sure of salvation.

Good Friday