Date: 
04-11-2021
Reading: 
Luka 8:16-18

Alhamisi asubuhi 04.11.2021

Luka 8:16-18

[16]Hakuna mtu ambaye akiisha washa taa huifunika kwa chombo, au kuiweka mvunguni, bali huiweka juu ya kiango, ili waingiao wapate kuona nuru yake.

[17]Kwa maana hakuna neno lililositirika ambalo halitafunuliwa; wala lililofichwa ambalo halitajulikana na kutokea wazi.

[18]Jiangalieni basi jinsi msikiavyo; kwa kuwa mwenye kitu atapewa, na yule asiye na kitu atanyang’anywa hata kile ambacho anadhaniwa kuwa nacho.

 

Mwenye haki ataishi kwa imani;

Yesu alifundisha kwamba taa ikiwashwa hawekwi uvunguni, bali inawekwa juu ili kuangaza, na anasisitiza kuwa hakuna neno ambalo halitakuwa wazi;

Yesu anatufundisha nini asubuhi hii?

1. Tumepewa neema ya wokovu. Neema hii isiishie kwetu tu (tusiiweke uvunguni) bali tuwahubirie wengine kuhusu wokovu, ili katika haki nao waishi kwa imani.

2. Hakuna jambo unalofanya ambalo Mungu halijui wala halioni. Uzinzi unaofanya, rushwa unayokula, wizi wako, utapeli, uongo n.k vyote vinajulikana kwa Mungu. Matendo yote hayo yatafunuliwa wazi, na hutaurithi ufalme wa Mungu. Tubu sasa, ubadilike. Fanya matengenezo katika maisha yako. 

3. Tufanye kazi kwa bidii. Uvivu ni dhambi. Tumewekwa duniani kumtumikia Mungu tukifanya kazi. Ukiwa mvivu hata hicho kidogo utanyang'anywa. Yaani mtafute Mungu kwa bidii, ili upate nafasi ya kuingia katika ufalme wake. Ukimtafuta kwa wasiwasi hautamuona (hata hicho kidogo utanyang'anywa).

Tunaitwa kuishi kwa imani, maisha yetu yakimshuhudia Kristo kama Mwokozi wa ulimwengu.

Siku njema.