Date: 
12-04-2022
Reading: 
Kutoka 6:1-8

Juma Takatifu;

Jumanne asubuhi tarehe12.04.2022

Kutoka 6:1-8

1 Bwana akamwambia Musa, Sasa utaona nitakavyomtenda Farao; maana kwa mkono hodari atawapa ruhusa kwenda zao, na kwa mkono hodari atawafukuza katika nchi yake.

2 Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA;

3 nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.

4 Tena nimelithibitisha agano langu nao, la kuwapa nchi ya Kanaani; nchi ya kukaa kwao hali ya ugeni.

5 Na zaidi ya hayo, nimesikia kuugua kwao wana wa Israeli, ambao Wamisri wanawatumikisha, nami nimelikumbuka agano langu.

6 Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni YEHOVA, nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya mizigo ya Wamisri, nami nitawaokoa na utumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu kubwa;

7 nami nitawatwaeni kuwa watu wangu, nitakuwa Mungu kwenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ni YEHOVA, Mungu wenu, niwatoaye mtoke chini ya mizigo ya Wamisri.

8 Nami nitawaleta hata nchi ile ambayo naliinua mkono wangu, niwape Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo; nitawapa iwe urithi wenu; Mimi ni YEHOVA.

Hosana ndiye mbarikiwa;

Ajaye kwa jina la Bwana.

Farao hakutaka Israeli waondoke Misri. Hakujua asingeweza kushindana na Bwana. Somo la leo asubuhi linaonesha Mungu akimpa tumaini na kumhakikishia Musa kuwa Israeli wataondoka Misri kwa neema ya Mungu. Bwana anaahidi kuwa atawatwaa Israeli kutoka Misri, na kuwapa nchi ya ahadi.

Mungu aliyeahidi kuwaokoa Israeli toka mikononi mwa Farao, anatuahidi kutuokoa sisi toka kwenye dhambi na uovu wa ulimwengu huu. Wajibu wetu ni kumpokea Yesu, aingie mioyoni mwetu na kutusafisha akituondolea dhambi zetu, ili tudumu katika yeye kwa ajili ya uzima wetu, sasa na hata milele.

Siku njema.