Date: 
28-01-2022
Reading: 
Kumbukumbu la Torati 10:12-21

Ijumaa asubuhi tarehe 28.01.2022

Kumbukumbu la Torati 10:12-21

12 Na sasa, Israeli, Bwana, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche Bwana, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote;

13 kuzishika amri za Bwana na sheria zake, ninazokuamuru leo, upate uheri?

14 Tazama, mbingu ni mali za Bwana, Mungu wako, na mbingu za mbingu, na nchi, na vitu vyote vilivyomo.

15 Tena, Bwana aliwafurahia baba zako, na kuwapenda, akawachagua wazao wao baada yao, naam, na ninyi zaidi ya mataifa yote kama hivi leo.

16 Basi, zitahirini govi za mioyo yenu, wala msiwe na shingo ngumu.

17 Kwa maana Bwana, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, asiyependelea nyuso za watu, wala hakubali rushwa.

18 Huwafanyia yatima na mjane hukumu ya haki, naye humpenda mgeni, akimpa chakula na mavazi.

19 Basi, mpendeni mgeni, kwa sababu ninyi wenyewe mlikuwa wageni katika nchi ya Misri.

20 Mche Bwana, Mungu wako, umtumikie yeye; ambatana naye, na kuapa kwa jina lake.

21 Yeye ndiye fahari yako, na yeye ndiye Mungu wako, aliyekutendea mambo haya makubwa, ya kutisha, uliyoyaona kwa macho yako.

Mungu anaondoa ubaguzi;

Asubuhi hii tunasoma juu ya ujumbe wa Mungu kwa taifa lake juu ya kumcha, kumpenda, na kumtumikia kwa akili, roho na moyo wote. Anawaamuru watu wake kuzishika amri zake ili wapate heri. Anawahakikishia kuwa yeye ni mwenye hukumu za haki.

Mungu anatuma ujumbe kwa Israeli "wote" na siyo baadhi. Tafsiri yake ni kuwa neno la Mungu ni kwa ajili ya watu wote. Halichagui, halibagui. Tabia hiyo ya Mungu, ndiyo tunayoitwa kuifuata, yaani tusiwe na ubaguzi kati yetu.

Siku njema.