VIJANA 13 WAPATA KIPAIMARA

Vijana ambao walikuwa wanafunzi wa Sunday school, siku ya Jumamosi tarehe 21.11.2015 walibarikiwa rasmi kuanza kuhudhuria ibada ya watu wazima baada ya kufuzu mafunzo ya kipaimara waliyosoma kwa muda wa mika miwili, Msaidizi wa Askofu Chediel Lwiza ndie aliyeongoza ibada hiyo akishirikiana na na Mchungaji Kiongozi Charles Mzinga, na Mchungaji Prudence Chuwa.

Mch. Lwiza alisema "Kuanzia leo mtakuwa mnaongozana na wazazi wenu na kuingia nao katika ibada ya watu wazima. Sasa, mnachotakiwa kiukifanya ni kujifunza neno la mungu na kulijua, mkikwama muonane na mchungaji ama waalimu wenu wa zamani wa sunday school, pia mnatakiwa kujiunga na kwaya mbalimbali ambazo zinahudumu hapa kanisani kwa sababu nyinyi sio watoto tena bali ni vijana"

Ibada hiyo pia ilihudhuriwa na wazazi na walezi, walimu wa sunday school na washarika mbalimbali.

Pia katika ibada hiyo kulikuwa na ubatizo wa mtoto mdogo mmoja na vijana wawili. Mambo yalikua kama ifuatavyo katika picha.

Msaidizi wa Askofu Mch. Chediel Lwiza, Mch. Prudence Chuwa, Mch. Kiongozi Charles Mzinga na watoto wakiingia ibadani kwa maadamano
Vijana waliohitimu mafunzo ya kipaimara wakifuatilia ibada
Vijana walioitimu mafunzo ya kipaimara wakifutilia ibada