Date: 
13-02-2020
Reading: 
Joshua 2:1-7

THURSDAY 13TH FEBRUARY 2020  MORNING                                                    

Joshua 2:1-7 New International Version (NIV)

Then Joshua son of Nun secretly sent two spies from Shittim. “Go, look over the land,” he said, “especially Jericho.” So they went and entered the house of a prostitute named Rahab and stayed there.

The king of Jericho was told, “Look, some of the Israelites have come here tonight to spy out the land.” So the king of Jericho sent this message to Rahab: “Bring out the men who came to you and entered your house, because they have come to spy out the whole land.”

But the woman had taken the two men and hidden them. She said, “Yes, the men came to me, but I did not know where they had come from. At dusk, when it was time to close the city gate, they left. I don’t know which way they went. Go after them quickly. You may catch up with them.” (But she had taken them up to the roof and hidden them under the stalks of flax she had laid out on the roof.) So the men set out in pursuit of the spies on the road that leads to the fords of the Jordan, and as soon as the pursuers had gone out, the gate was shut.

Rahab was not rescued by her works, but by her faith.  She knew who God was, she knew who she was, and she trusted God for her very life.

God's hand is not short to save people like Rahab, and He can work in amazing ways to bring salvation.


ALHAMISI TAREHE 13 FEBRUARI  2020  ASUBUHI                             

YOSHUA 2:1-7

1 Yoshua, mwana wa Nuni, akawatuma watu wawili kutoka Shitimu kwa siri, ili kupeleleza, akawaambia, Enendeni mkaitazame nchi hii, na Yeriko. Wakaenda wakafika nyumbani kwa kahaba mmoja jina lake aliitwa Rahabu, wakalala huko.
Mfalme wa Yeriko akaambiwa, kusema, Tazama, watu wawili wa wana wa Israeli wameingia humu leo usiku, ili kuipeleleza nchi.
Mfalme wa Yeriko akatuma watu kwa Rahabu, akasema, Watoe watu wale waliokuja kwako, walioingia ndani ya nyumba yako, maana wamekuja ili kuipeleleza nchi.
Yule mwanamke akawatwaa wale watu wawili, akawaficha, akasema, Naam, wale watu walikuja kwangu, lakini sikujua walikotoka;
ikawa kama wakati wa kufungwa lango la mji, kulipokuwa giza, watu wale wakatoka, wala sijui walikokwenda; wafuateni upesi, maana mtawapata.
Lakini yeye alikuwa amewapandisha darini, akawaficha kwa mabua ya kitani, aliyokuwa ameyatandika juu ya dari.
Basi hao watu wakawafuata kwa njia iendayo Yordani mpaka vivukoni; na mara wale watu waliowafuatia walipokwisha kutoka, wakalifunga lango.

Rahabu hakuokolewa kwa sababu ya matendo yake, bali kwa imani yake.  Alifahamu uweza wa Mungu, pia alijitambua kuwa yeye ni mtu wa namna gani; na akamtumaini Mungu kwa ajili ya maisha yake.

Mkono wa Mungu hauwezi kupungua hata usiweze kuokoa watu kama Rahabu, na pia anaweza kuleta wokovu katika namna ya kushangaza.