Date: 
23-07-2020
Reading: 
John 8:1-11 (Yohana 8:1-11)

THURSDAY 23RD JULY 2020     MORNING                                                                 

John 8:1-11  New International Version (NIV)

but Jesus went to the Mount of Olives.

At dawn he appeared again in the temple courts, where all the people gathered around him, and he sat down to teach them. The teachers of the law and the Pharisees brought in a woman caught in adultery. They made her stand before the group and said to Jesus, “Teacher, this woman was caught in the act of adultery. In the Law Moses commanded us to stone such women. Now what do you say?” They were using this question as a trap, in order to have a basis for accusing him.

But Jesus bent down and started to write on the ground with his finger. When they kept on questioning him, he straightened up and said to them, “Let any one of you who is without sin be the first to throw a stone at her.” Again he stooped down and wrote on the ground.

At this, those who heard began to go away one at a time, the older ones first, until only Jesus was left, with the woman still standing there. 10 Jesus straightened up and asked her, “Woman, where are they? Has no one condemned you?”

11 “No one, sir,” she said.

“Then neither do I condemn you,” Jesus declared. “Go now and leave your life of sin.”

This woman was not condemned by Christ, but he was condemned on the cross for her sake.

By God’s grace, we are saved and forgiven. We should let that grace change our lives.” We do not change in order to be accepted; we change because we have already been accepted. The grace received into the heart creates a new life to the one who believes.


ALHAMISI  TAREHE 23 JUNE 2020      ASUBUHI                                          

YOHANA 8:1-11

1 Walikwenda kila mtu nyumbani kwake; naye Yesu akaenda mpaka mlima wa Mizeituni.
Hata asubuhi kulipokucha akaingia tena hekaluni, na watu wote wakamwendea; naye akaketi, akawa akiwafundisha.
Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati.
Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini.
Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje?
Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi.
Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.
Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi.
Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati.
10 Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia?
11 Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.]

Mwanamke huyu hakuhukumiwa na Yesu, lakini Yesu alihukumiwa msalabani kwa ajili yake.

Kwa neema ya Mungu tumeokolewa na kusamehewa. Tunahitaji kuruhusu neema hiyo iyabadili maisha yetu. Hatubadiliki ili tuweze kukubalika na Mungu; tunabadilika kwa sababu tayari tulishakubaliwa na Mungu. Neema iliyopokelewa moyoni huleta maisha mapya kwake yeye aminiye.