Date: 
14-06-2021
Reading: 
John 5:22-24 (Yohana)

MONDAY 14TH JUNE 2021, MORNING       

John 5:22-24 New International Version (NIV)

22 Moreover, the Father judges no one, but has entrusted all judgment to the Son, 23 that all may honor the Son just as they honor the Father. Whoever does not honor the Son does not honor the Father, who sent him.

24 “Very truly I tell you, whoever hears my word and believes him who sent me has eternal life and will not be judged but has crossed over from death to life.

God gave all judgment to Jesus, who is the second Adam, and in this case, He is returning Man into his original position on earth, with dominion over all creation, as determined before man fell.

Sinners saved by grace through faith in Him know that the judgment we deserve, as payment for our sin, was fully paid at the cross. Moreover, Christ has pronounced us redeemed by His own, precious blood. He has prepared a place for us to be with Him in the heavenly Kingdom, if we truly submit to His will and live out our faith; and be a person for others.


JUMATATU TAREHE 14 JUNI 2021,  ASUBUHI                              

YOHANA 5:22-24 

22 Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote;
23 ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba aliyempeleka.
24 Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.

Mungu alimpa Yesu hukumu yote, yeye aliye Adamu wa pili; na kwa hali hii, anamrejeshea mwanadamu nafasi yake ya asili hapa duniani, kutawala viumbe vyote, kama ilivyokuwa kabla ya anguko la mwanadamu.

Wenye dhambi waliookolewa kwa imani kwa njia ya Kristo wanatambua kuwa hukumu waliyostahili, kama malipo ya dhambi zetu, ililipwa kwa ukamilifu pale msalabani. Zaidi ya hayo, Kristo ametuhakikishia ukombozi kwa damu yake ya thamani. Naye ameandaa makao kwa ajili yetu ili tuweze kuwa naye katika Ufalme wa Mbinguni, ikiwa tutafuata mapenzi yake na kuishi imani yetu, huku tukitumikiana sisi kwa sisi.