Date: 
30-05-2020
Reading: 
Jeremiah 14:7-9

SATURDAY 30TH MAY 2020    MORNING 

Jeremiah 14:7-9 New International Version (NIV)

Although our sins testify against us,
do something, Lord, for the sake of your name.
For we have often rebelled;
    we have sinned against you.
8 You who are the hope of Israel,
    its Savior in times of distress,
why are you like a stranger in the land,
    like a traveler who stays only a night?
9 Why are you like a man taken by surprise,
    like a warrior powerless to save?
You are among us, Lord,
    and we bear your name;
    do not forsake us!

When God bring discipline or judgment to the land, it also affects the whole creation around us. Our sincere and constant repentance would not only benefit us, but also the natural world.

Let us come to God with humility and repentance, seeking to remind Him that He is our only hope and savior. 


JUMAMOSI TAREHE 30 MAY 2020      ASUBUHI                          YEREMIA 14:7-9

7 Ijapokuwa maovu yetu yanatushuhudia, lakini utende wewe kwa ajili ya jina lako, Ee Bwana, maana kurudi nyuma kwetu ni kwingi; tumekutenda dhambi.
8 Wewe uliye tumaini la Israeli, wewe uliye Mwokozi wake wakati wa taabu, kwa nini wewe umekuwa kama mtu akaaye katika nchi, hali ya mgeni, na kama mtu mwenye kusafiri, ageukaye upande ili kukaa usiku mmoja tu?
9 Kwa nini wewe umekuwa kama mtu aliyesituka, kama shujaa asiyeweza kuokoa? Lakini wewe, Bwana, u katikati yetu, nasi tunaitwa kwa jina lako; usituache.

Mungu anapoleta adhabu au hukumu juu ya nchi, madhara yake hugusa uumbaji wote unaotuzunguka. Tukimwendea Mungu kwa toba ya kweli na kujitakasa kila wakati, haitatusaidia sisi tu, bali uumbaji wote utabadilika. 

Twende mbele za Mungu kwa unyenyekevu na toba, tukitafuta kumkumbusha kuwa yeye Mungu ndiye tumaini pekee na ukombozi wetu.