Date: 
03-02-2023
Reading: 
Isaya 8:19-22

Ijumaa asubuhi tarehe 03.02.2023

Isaya 8:19-22

[19]Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong’ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai?

[20]Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.

[21]Nao watapita katikati yake, wamedhikika sana na kuwa na njaa; na itakuwa watakapoona njaa, watalalamika na kuapa kwa mfalme wao, na kwa Mungu wao, na kuelekeza nyuso zao juu;

[22]nao wataiangalia nchi, na, tazama, shida na giza; hapana changamko kwa sababu ya dhiki; nao watafukuzwa na kuingia katika giza kubwa.

Kung'aa kwa Yesu Kristo;

Nabii Isaya anaongea na wale waliokuwa wakimsikiliza na kumfuata wakati wa huduma yake. Anawataka kwenda sawa na ushuhuda wa neno la Mungu. Isaya anaandika akionesha kuwa kuenenda kwa ushuhuda siyo jambo rahisi. Mstari wa 21 na 22 inataja kwamba shida, njaa na dhiki zinawakuta wamfutao Bwana.

Hivyo Isaya hapa anaonesha kwamba kumfuata Bwana siyo kazi rahisi, imejaa vikwazo. 

Sura ya 8 inaishia hapa kwenye somo la asubuhi hii. Sasa ukiendelea na sura ya 9 ndipo unakuta Isaya akitabiri Ujio wa Yesu Kristo. Mstari wa 6 unamtaja Yesu Kristo kama mfalme ajaye;

Isaya 9:6

[6]Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, 
Tumepewa mtoto mwanamume; 
Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; 
Naye ataitwa jina lake, 
Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, 
Baba wa milele, Mfalme wa amani.

Yesu Kristo kama alivyotabiriwa na Isaya ndiye hutuongoza kushinda katikati ya shida, giza na dhiki kama tulivyosoma kwenye somo letu la leo asubuhi. Kung'aa kwake ilikuwa kutuweka imara, kwamba tunaye kiongozi ambaye tukimtegemea hutuwezesha kushinda katikati ya majaribu, na hatimaye kutupa uzima wa milele.

Ijumaa njema 

Heri Buberwa