Date: 
16-12-2021
Reading: 
Isaya 56:1-7

Hii ni Advent 

Alhamisi asubuhi tarehe16.12.2021

Isaya 56:1-7

1 Bwana asema hivi, Shikeni hukumu, mkatende haki; kwa maana wokovu wangu u karibu kuja, na haki yangu kufunuliwa.

2 Heri afanyaye haya, na mwanadamu ayashikaye sana; azishikaye sabato asizivunje, auzuiaye mkono wake usifanye uovu wo wote.

3 Wala mgeni, aambatanaye na Bwana, asiseme hivi, Hakika yake Bwana atanitenga na watu wake; wala towashi asiseme, Mimi ni mti mkavu.

4 Kwa maana Bwana awaambia hivi matowashi, wanaozishika sabato zangu, na kuyachagua mambo yanipendezayo, na kulishika sana agano langu;

5 Nitawapa hawa nyumbani mwangu, na ndani ya kuta zangu, kumbukumbu na jina, lililo jema kuliko kuwa na wana na binti; nitawapa jina lidumulo milele, lisilokatiliwa mbali.

6 Na wageni, walioandamana na Bwana ili wamhudumu, na kulipenda jina la Bwana, kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu;

7 Nitawaleta hao nao hata mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote.

Itengenezeni njia ya Bwana;

Isaya analeta ujumbe wa kulishika neno la Mungu kwa kutenda haki. Anakazia kuwa heri alishikaye neno la Mungu pasipo kufanya uovu. Anatuita kumcha Bwana kwa ibada na sadaka zetu hekaluni mwake, maana nyumba yake ni nyumba ya sala.

Tunaitwa kulishika neno la BWANA tukitenda haki, maana itatuondolea hukumu ya adhabu ya milele. Ibada na matendo mema ni muhimu tunapomngojea Kristo kurudi kwa mara ya pili. Bwana akubariki, ukiwa na siku njema.