Date: 
25-02-2022
Reading: 
Isaya 55:8-11

Ijumaa asubuhi; tarehe 25.02.2022

Isaya 55:8-11

8 Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana.

9 Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.

10 Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula;

11 ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.

Neno la Mungu lina nguvu;

Mungu kupitia nabii Isaya anaonesha kuwa ni mkuu, halinganishwi na mwanadamu, wala kitu chochote. Wakati sisi tukiwaza yanayotuhusu, yeye huwaza juu ya wokovu kwa ulimwengu wote. Hapo anaonesha kwamba sisi ni watu wake, tunaotakiwa kuishi kwa kumtegemea yeye.

Ujumbe wa asubuhi hii uko katika mstari wa 11, pale Mungu anapoonesha kuwa amelitoa neno lake kwa ajili ya ulimwengu. Mungu ametupa neno lake ili tulishike na kumfuata, ili mapenzi yake yatimizwe katika kuokoa ulimwengu.

Siku njema.