Date: 
22-11-2022
Reading: 
Isaya 52:1-6

Jumanne asubuhi tarehe 22.11.2022

Isaya 52:1-6

[1]Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Sayuni; 

Jivike mavazi yako mazuri, 

Ee Yerusalemu, mji mtakatifu; 

Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako 

Asiyetahiriwa, wala aliye najisi.

[2]Jikung’ute mavumbi; uondoke, 

Uketi, Ee Yerusalemu; 

Jifungulie vifungo vya shingo yako, 

Ee binti Sayuni uliyefungwa.

[3]Maana BWANA asema hivi, Mliuzwa bure; nanyi mtakombolewa bila fedha.

[4]Maana Bwana MUNGU asema hivi, Watu wangu hapo kwanza walishuka Misri ili wakae huko hali ya ugeni; na Mwashuri akawaonea bila sababu.

[5]Basi sasa, nafanya nini hapa, asema BWANA, ikiwa watu wangu wamechukuliwa bure? Hao wanaowatawala wanapiga yowe, asema BWANA, na jina langu linatukanwa daima mchana kutwa.

[6]Kwa hiyo watu wangu watalijua jina langu kwa hiyo watajua siku ile ya kuwa mimi ndimi ninenaye; tazama ni mimi.

Uzima wa ulimwengu ujao;

Nabii Isaya anauongelea mji Mtakatifu ambao hakitaingia kitu chochote kilicho najisi. Kwa kukazia anaanza na maneno amka, amka... aina hii ya maneno imetumika sana kwenye Biblia pale mkazo na(au) msisitizo ulipotakiwa. Mfano, Yesu kuna wakati alisema, Amin, Amin nawaambia....

Isaya anatoa picha ya ukombozi wa wana wa Israeli toka utumwani Misri, akionesha kwamba mpango wa Mungu siku zote ni ukombozi.

Ujumbe tunaoupata asubuhi hii ni kuwa mbingu ni ya waaminio, waliomwamini Yesu na kutenda mema. Hataingia huko mtu ambaye hakumcha Bwana maishani mwake. Mpango wa Mungu ni ukombozi kwa wanadamu, waliomkubali wakamwamini na kumpokea. 

Siku njema.