Date: 
09-12-2021
Reading: 
Isaya 24:18-52

Hii ni Advent 

Alhamisi asubuhi tarehe 09.12.2021

Isaya 28:14-22

[14]Basi, lisikieni neno la BWANA, enyi watu wenye dharau, mnaowatawala watu hawa walio ndani ya Yerusalemu.

[15]Kwa sababu mmesema, Tumefanya agano na mauti, tumepatana na kuzimu; pigo lifurikalo litakapopita, halitatufikia sisi; kwa maana tumefanya maneno ya uongo kuwa kimbilio letu, tumejificha chini ya maneno yasiyo kweli;

[16]kwa ajili ya hayo Bwana, MUNGU, asema hivi, Tazama, naweka jiwe katika Sayuni, liwe msingi, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni lenye thamani, msingi ulio imara; yeye aaminiye hatafanya haraka.

[17]Nami nitafanya hukumu kuwa ndiyo kanuni, na haki kuwa ndiyo timazi; na mvua ya mawe itachukulia mbali hilo kimbilio la maneno ya uongo, na maji yatapagharikisha mahali pa kujisitiri.

[18]Na agano lenu mliloagana na mauti litabatilika, tena mapatano yenu mliyopatana na kuzimu hayatasimama; pigo lifurikalo litakapopita, ndipo ninyi mtakapokanyagwa nalo.

[19]Kila wakati litakapopita litawachukueni. Maana litapita asubuhi baada ya asubuhi, wakati wa mchana na wakati wa usiku; na kuifahamu habari ile kutakuwa kitisho tu.

[20]Maana kitanda kile ni kifupi asiweze mtu kujinyosha juu yake, na nguo ile ya kujifunika ni nyembamba asipate mtu kujizingisha.

[21]Maana BWANA ataondoka kama vile katika mlima Perasimu, ataghadhibika kama vile katika bonde la Gibeoni; apate kufanya kazi yake, kazi yake ya ajabu; na kulitimiza tendo lake, tendo lake la ajabu.

[22]Basi sasa msiwe watu wenye kudharau, vifungo vyenu msije vikakazwa; maana nimesikia kwa Bwana, BWANA wa majeshi, habari ya hukumu itakayotimizwa, nayo imekusudiwa, itakayoipata dunia yote pia.

Bwana anakuja katika Ufalme wake;

Isaya analeta ujumbe juu ya hukumu kwa watawala mafisadi, makuhani na manabii. Anajenga picha ya watu waliokabidhiwa mamlaka bila kutenda haki kuadhibiwa.

Kwa Kanisa la leo, kila mmoja wetu popote alipo amepewa wajibu wake. Ni wajibu wa kila mmoja wetu kuitenda kazi yake kwa uaminifu pale alipo, maana kwa kufanya hivyo unamwakilisha Mungu. Kutotimiza wajibu wako ni dhambi itakayosababisha uukose uzima wa milele.

Siku njema.