Date: 
07-12-2021
Reading: 
Isaya 11:1-9

Hii ni Advent 

Jumanne asubuhi tarehe 07.12.2021

Isaya 11:1-9

[1]Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda.

[2]Na roho ya BWANA atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha BWANA;

[3]na furaha yake itakuwa katika kumcha BWANA; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake;

[4]bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya.

[5]Na haki itakuwa mshipi wa viuno vyake, na uaminifu mshipi wa kujifungia.

[6]Mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwana-simba na kinono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza.

[7]Ng’ombe na dubu watalisha pamoja; watoto wao watalala pamoja; na simba atakula majani kama ng’ombe.

[8]Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la nyoka, na mtoto aliyeachishwa atatia mkono wake katika pango la fira.

[9]Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima wangu wote mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua BWANA, kama vile maji yanavyoifunika bahari.

Bwana anakuja katika Ufalme wake;

Isaya anatabiri ujio wa Yesu kama mfalme mwenye amani atakayetawala kwa haki. Isaya alitabiri Yesu kuwa mwenye Roho wa Mungu, ambaye angekuja kuleta wokovu.

Isaya alitabiri kuja kwa Yesu, na Yesu alikuja kama mtawala na mfalme. Yesu huyu huyu atarudi kwa utukufu kulichukua Kanisa kama alivyosema. Umejiandaaje kumpokea?

Siku njema.