Date: 
09-05-2019
Reading: 
Isaiah 57:7-10

THURSDAY 9TH MAY 2019 MORNING                                        
Isaiah 54:7-10 New International Version (NIV)
7 “For a brief moment I abandoned you,
    but with deep compassion I will bring you back.
8 In a surge of anger
    I hid my face from you for a moment,
but with everlasting kindness
    I will have compassion on you,”
    says the Lord your Redeemer.
9 “To me this is like the days of Noah,
    when I swore that the waters of Noah would never again cover the earth.
So now I have sworn not to be angry with you,
    never to rebuke you again.
10 Though the mountains be shaken
    and the hills be removed,
yet my unfailing love for you will not be shaken
    nor my covenant of peace be removed,”
    says the Lord, who has compassion on you.


Many times the Israelites rebelled against God. They failed to obey His laws and they worshipped idols. God punished them for a while but when they repented he had compassion on them and forgave their sins and gave them peace.
God is merciful to us and forgiving. Let us trust in Him and obey His laws. When we fall into sin we need to come back to God quickly and repent our sins and ask for His help to obey Him. 


ALHAMISI TAREHE 9 MEI 2019 ASUBUHI                                        
Isaya 54:7-10
7 Kwa kitambo kidogo nimekuacha; lakini kwa rehema nyingi nitakukusanya. 
8 Kwa ghadhabu ifurikayo nalikuficha uso wangu dakika moja; lakini kwa fadhili za milele nitakurehemu, asema Bwana, Mkombozi wako. 
9 Kwa maana jambo hili limekuwa kama maji ya Nuhu kwangu; maana kama nilivyoapa ya kwamba maji ya Nuhu hayatapita juu ya dunia tena, kadhalika nimeapa ya kwamba sitakuonea hasira, wala kukukemea. 
10 Maana milima itaondoka, na vilima vitaondolewa; bali wema wangu hautaondoka kwako, wala agano langu la amani halitaondolewa; asema Bwana akurehemuye. 

Mara kwa mara Waisraeli walimwaasi Mungu. Walivunja amri zake na kuabudu sanamu. Mungu aliwapa adhabu kwa muda ili wamrejee. Walipotubu na kumrejea Mungu aliwasamehe na kuwahurumia na kuwabariki tena.
Labda sisi tuko kama Waisraeli. Labda tumetenda dhambi au upendo wetu kwa Mungu u?mepoa. Tutubu dhambi zetu upesi na kurejea kwa Mungu wetu. Atatuhurumia na kutubariki. Omba Mungu akupe neema kutembea naye kila siku ya maisha yako.