Date: 
23-12-2019
Reading: 
Isaiah 2:2-5

MONDAY 23RD DECEMBER 2019 MORNING 
Isaiah 2:2-5 New International Version (NIV)
2 In the last days
the mountain of the Lord’s temple will be established
    as the highest of the mountains;
it will be exalted above the hills,
    and all nations will stream to it.
3 Many peoples will come and say,
“Come, let us go up to the mountain of the Lord,
    to the temple of the God of Jacob.
He will teach us his ways,
    so that we may walk in his paths.”
The law will go out from Zion,
    the word of the Lord from Jerusalem.
4 He will judge between the nations
    and will settle disputes for many peoples.
They will beat their swords into plowshares
    and their spears into pruning hooks.
Nation will not take up sword against nation,
    nor will they train for war anymore.
5 Come, descendants of Jacob,
    let us walk in the light of the Lord.


Christians are called to strengthen one another, and support one another. It is God who teaches his people, by his word and Spirit. In this Advent season, Christ is coming into our lives to promote peace, as well as holiness through the renewal of our hearts and minds. 
    


JUMATATU TAREHE 23 DESEMBA 2019  ASUBUHI                                                     ISAYA 2:2-5
2 Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi.
3 Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana katika Yerusalemu.
4 Naye atafanya hukumu katika mataifa mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.
5 Enyi wa nyumba ya Israeli, njoni, twende katika nuru ya Bwana.

Wakristo tunahimizwa kuimarishana, na kusaidiana. Mungu ndiye afundishaye watu wake, kwa neno na kwa roho. Katika majira haya ya Majilio, Kristo anakuja maishani mwetu kuhubiri amani pamoja na utakatifu; kwa njia ya kuhuisha mioyo na akili zetu.