Date: 
03-12-2021
Reading: 
Hesabu 15:37-41

Hii ni Advent:

Ijumaa asubuhi tarehe 03.12.2021

Hesabu 15:37-41

37 Kisha BWANA akasema na Musa, na kumwambia,

38 Nena na wana wa Israeli, na kuwaagiza ya kwamba wajifanyie vishada katika ncha za nguo zao, katika vizazi vyao, tena ya kwamba watie katika kila kishada cha kila ncha nyuzi za rangi ya samawi;

39 nacho kitakuwa kwenu ni kishada, ili mpate kukiangalia, na kuyakumbuka maagizo yote ya BWANA, na kuyafanya; tena kwamba msiende kutanga-tanga kuandama mioyo yenu wenyewe, na macho yenu wenyewe, ambayo mlikuwa mkiyaandama kwa uasherati hapo kwanza;

40 ili mpate kukumbuka na kuyafanya maagizo yangu yote, na kuwa watakatifu kwa Mungu wenu.

41 Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili kwamba niwe Mungu wenu; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.

Bwana analijia Kanisa lake;

Mungu anawaambia Israeli kuyashika maagizo yake, waache kutangatanga. Anawaita kukaa katika utakatifu wakimcha yeye, maana yeye ndiye mkombozi wao aliyewatoa Misri.

Vivyo hivyo Mungu anatuita kumcha yeye. Anatuzuia kutangatanga, akitutaka kukaa kwake maana ndiyo sehemu sahihi kwa ajili ya hatma yetu. Kaa kwa Yesu, maana ndiko kuna hatma yako. 

Siku njema.