Date: 
08-08-2019
Reading: 
Hebrews 12:14-16

THURSDAY  8TH AUGUST 2019   MORNING                   
Hebrews 12:14-16 New International Version (NIV)

Warning and Encouragement


14 Make every effort to live in peace with everyone and to be holy; without holiness no one will see the Lord. 15 See to it that no one falls short of the grace of God and that no bitter root grows up to cause trouble and defile many. 16 See that no one is sexually immoral, or is godless like Esau, who for a single meal sold his inheritance rights as the oldest son.

This Epistle is written to Christians from a Jewish  background.  Biblical scholars are not sure who the author is. It contains much explanation as to how the Jewish faith in completed by the Gospel.
In the above passage we read general advice about Christian Ethics.  God would like us to live a Holy life. Let us try to live to please God.

   


ALHAMISI  TAREHE 8 AGOSTI 2019 ASUBUHI
Waebrania 12:14-16


14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; 
15 mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo. 
16 Asiwepo mwasherati wala asiyemcha Mungu, kama Esau, aliyeuuza urithi wake wa mzaliwa wa kwanza kwa ajili ya chakula kimoja. 

  
Watalamu wa Biblia hawana uhakika kuhusu mwandishi wa Waraka kwa Waebrania. Lakini wanajua iliandikwa kwa Wakristo ambao walitoka kwenye asili ya Kiyahudi. Waraka huu ina maelezo mengi kuhusu Utaratibu za dini ya Kiyahudi na jinsi zina kamilishwa katika Injili.   
Mistari hapa juu inatukumbusha kuhusu maadili ya Kikristo. Mungu atusaidia kuishi maisha takatifu kumpendeza Mungu.