Date: 
07-11-2018
Reading: 
Hebrews 12:1-3 (Waebrania 12:1-3)

WEDNESDAY 7TH NOVEMBER 2018

Hebrews 12:1-3 New International Version (NIV)

1 Therefore, since we are surrounded by such a great cloud of witnesses, let us throw off everything that hinders and the sin that so easily entangles. And let us run with perseverance the race marked out for us, fixing our eyes on Jesus, the pioneer and perfecter of faith. For the joy set before him he endured the cross, scorning its shame, and sat down at the right hand of the throne of God. Consider him who endured such opposition from sinners, so that you will not grow weary and lose heart.

In following Jesus, there will be challenges, but the verses above from St. Paul give us courage to carry on looking at Christ as our beacon, as he endured the shame and pain on the cross and now sits on the right hand of God. Pray that God gives you the courage to focus on Christ in your trials and tribulations.

JUMATANO TAREHE 7 NOVEMBA 2018

Waebrania 12:1-3

1 Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,
2 tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.
3 Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili mapingamizi makuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu.

Katika kumfuata Yesu, kutakuwa na changamoto, lakini mistari ya juu kutoka kwa Mtume Paulo inatupa ujasiri wa kuendelea kumtazama Kristo kama nguzo yetu, kwani alivumilia aibu na maumivu msalabani, na sasa ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Omba ili Mungu akupe ujasiri wa kumtazama Kristo katika majaribu na mateso yako.