Tukio hilo lilifanyika kanisani Azania katika ibada zote 2 za kiswahili likiongozwa na Msaidizi wa Askofu Dean
George Fupe akisidiana na Chaplain Charles Mzinga. Kabla ya harambee, video fupi inayoonyesha maendeleo
ya mradi ulipofikia ilionyeshwa. Chaplain Mzinga alisema lengo la harambee hiyo ni kukusanya jumla ya
Shilingi 300 milioni ili kufikia bajeti ya Sh. 700 milioni zinazohitajika kukidhi zoezi lakuezeka paa la jengo la
mikutano, ambalo ndio awamu ya kwanza ya mradi. Aidha paa hilo la iana yake, litatengenezwa China na kuja
kuunganishwa kwenye jengo Kiharaka. Pia kitenge maalum kwa ajili ya kuchangia mradi kiliwekwa wakfu na
Dean Fupe, na kunadiwa. Ushiriki wa washarika ulikuwa mzuri, wote walipewa nafasi yakushiriki kwa jinsi nafsi
zao zilivyowasukuma. Pia tulibarikiwa sana namahubiri ya Mch. Richard Hanaja wa KKKT Kigogo, aliyetoa mahubiri
ya siku hiyo. Kichwa cha Neno kilikuwa "Utoaji wa Kikristo" 2 Wakorintho 1-5
Dean Fupe akizindua harambee katika ibada ya kwanza
Wazee wa usharika waliokuwapo waliongoza kutoa ahadi zao katika ibada ya kwanza.
Washarika wa ibada ya kwanza wakifuatilia harambee kwa makini
Kitenge maalum kiliwekwa wakfu na kunadiwa
Msharika wa kwanza kununua kitenge kwa mnada.
Mzee wa usharika, Dr. Samwel Swai naye akipata kitenge.
Chaplain Mzinga akinadi kitenge
Wengi walichangamkia fursa ya kupata kitenge maalum.
Wazee Gody na Beatrice wakiwa katika kuweka mahesabu sawa huku harambee ikiendelea.
______________________________________________________________________________________________________________
Katika ibada ya pili, kwa sehemu mambo yalikuwa hivi...
Dean Fupe akihamasisha harambee
Injinia Kishimbo na mkewe wa KKKT Kijitonyama wakituunga mkono kwenye harambee.
Washarika H. Moshi na mkewe wakichangia
Mzee E. Moshi na Mama Mengi wakichangia harambee
Mzee T. Mlaki "mzee wa kiharaka" akichangia na wengine wakisubiri zamu yao.
Walikuwepo watu wa rika zote.
Mch. mstaafu Aston Kibona alikuwepo
Doris, Katibu wa Chaplain naye alikuwapo
Chaplain Mzinga akinadi Kitenge maalum ibada ya pili
Mzee Filemon Mgaya akichangia
Msharika akipata kitenge