Date: 
23-08-2022
Reading: 
Habakuki

Jumanne asubuhi 23.08.2022

Habakuki 1:1-4

[1]Ufunuo aliouona nabii Habakuki.

[2]Ee BWANA, nilie hata lini, wewe usitake kusikia? Nakulilia kwa sababu ya udhalimu, ila hutaki kuokoa.

[3]Mbona wanionyesha uovu, na kunitazamisha ukaidi? Maana uharibifu na udhalimu u mbele yangu; kuna ugomvi, na mashindano yatokea.

[4]Kwa sababu hiyo sheria imelegea, wala hukumu haipatikani; kwa maana watu wabaya huwazunguka wenye haki; kwa sababu hiyo hukumu ikipatikana imepotoka.

Tutumie vizuri nafasi tuliyopewa;

Nabii Habakuki anamlalamikia Bwana kwa kuwaacha watu wakionewa. Waliostahili haki hawakuipata. Jamii ilijaa ugomvi na mashindano, ambapo wenye nguvu walikuwa juu ya wanyonge. Jamii haikutenda haki kwa waliostahili, maana sheria hazikufuatwa. Watu wabaya waliwadhulumu wenye haki, hadi hukumu na maamuzi yakawa yenye upendeleo kwenye jamii.

Ukisoma sura ya pili, Habakuki sasa anasimama katika zamu yake kutafuta majibu ya malalamiko yake;

Habakuki 2:1

[1]Mimi nitasimama katika zamu yangu, nitajiweka juu ya mnara, nitaangalia ili nione atakaloniambia, na jinsi nitakavyojibu katika habari ya kulalamika kwangu.

Zipo changamoto nyingi katika familia zetu na jamii kwa ujumla. Suluhisho haliwezi kuwa kulalamika tu, bali kila mtu kutimiza wajibu wake. Tukimtegemea Mungu anatuongoza na kutuonesha jinsi ya kukabili na kutatua changamoto zinazotuzunguka. Simama katika zamu yako kushinda dhambi, ukitetea ukweli na haki ya Mungu kwa wote. Tumia vizuri nafasi uliyopewa.

Subiri kuhesabiwa hapo nyumbani.

Mapumziko mema.