Date: 
31-03-2020
Reading: 
Genesis 14:8-15 (Mwanzo 14:8-15)

TUESDAY 31ST MARCH 2020 MORNING                                       
Genesis 14:8-15 New International Version (NIV)


8 Then the king of Sodom, the king of Gomorrah, the king of Admah, the king of Zeboyim and the king of Bela (that is, Zoar) marched out and drew up their battle lines in the Valley of Siddim 9 against Kedorlaomer king of Elam, Tidal king of Goyim, Amraphel king of Shinar and Arioch king of Ellasar—four kings against five. 10 Now the Valley of Siddim was full of tar pits, and when the kings of Sodom and Gomorrah fled, some of the men fell into them and the rest fled to the hills. 11 The four kings seized all the goods of Sodom and Gomorrah and all their food; then they went away. 12 They also carried off Abram’s nephew Lot and his possessions, since he was living in Sodom.
13 A man who had escaped came and reported this to Abram the Hebrew. Now Abram was living near the great trees of Mamre the Amorite, a brother[b] of Eshkol and Aner, all of whom were allied with Abram. 14 When Abram heard that his relative had been taken captive, he called out the 318 trained men born in his household and went in pursuit as far as Dan. 15 During the night Abram divided his men to attack them and he routed them, pursuing them as far as Hobah, north of Damascus.

    
Abram and Lot parted each other due to the prevailing conflict between their herdsmen. Abram being wise gave Lot the opportunity to choose where to go. He chose to live in Sodom, the fertile yet sinful and dangerous area. 
Jesus Christ is the Peace Maker. When the war broke out and Lot his nephew captured, Abram did not consider the historical conflict between them, but took initiative with his family to go and rescued him.
The reconciling power of God in us gives us the ability to make peace with each other. 



JUMANNE TAREHE 31 MACHI 2020 ASUBUHI                          
MWANZO 14:8-15
8 Mfalme wa Sodoma, na mfalme wa Gomora, na mfalme wa Adma, na mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela, ndio Soari, wakatoka wakapanga vita panapo bonde la Sidimu;
9 wapigane na Kedorlaoma mfalme wa Elamu, na Tidali mfalme wa Goimu, na Amrafeli mfalme wa Shinari, na Arioko mfalme wa Elasari, wafalme wanne juu ya wale watano.
10 Na bonde la Sidimu lilikuwa limejaa mashimo ya lami. Nao wafalme wa Sodoma na Gomora wakakimbia, wakaanguka huko, nao waliosalia wakakimbia milimani.
11 Wakachukua mali zote za Sodoma na Gomora na vyakula vyao vyote, wakaenda zao.
12 Wakamtwaa Lutu, mwana wa nduguye Abramu, aliyekaa huko Sodoma, na mali yake, wakaenda zao.
13 Mtu mmoja aliyeponyoka akaenda, akampasha habari Abramu Mwebrania; naye amekaa panapo mialoni ya Mamre, yule Mwamori, ndugu ya Eshkoli, na ndugu ya Aneri, na hao walikuwa wamepatana na Abramu.
14 Abramu aliposikia ya kwamba nduguye ametekwa mateka, akawapa silaha vijana wake, waliozaliwa katika nyumba yake, watu mia tatu na kumi na wanane, akawafuata mpaka Dani.
15 Akajipanga apigane nao usiku, yeye na watumwa wake, akawapiga, akawafukuza mpaka Hoba, ulioko upande wa kushoto wa Dameski.

 

Abramu na Lutu nduguye walitengana kwa sababu ya ugomvi uliokuwa unaendelea kati ya watumishi waliochunga mifugo yao. Abramu kwa hekima alimpa nduguye nafasi ya kuchagua mahali popote apendapo ili aende huko. Lutu alichagua kuishi eneo la Sodoma, lililokuwa na ardhi nzuri yenye rutuba lakini pia uovu na hatari nyingi.  
Yesu Kristo ni Mpatanishi. Vita ilipotokea na Lutu nduguye Abramu kutekwa, Abramu hakutazama historia ya mgogoro uliowafanya kutengana, bali alichukua hatua, yeye na familia yake kwenda kupigana ili kumwokoa ndugu yake. 
Nguvu ya Mungu ya upatanisho iliyo ndani yetu inatupa uwezo wa kufanya upatanisho na wengine.