Date: 
19-08-2019
Reading: 
Deutoronomy 15:18-20

MONDAY 19TH AUGUST 2019 MORNING               
Deuteronomy 8:11-20 New International Version (NIV)
11 Be careful that you do not forget the Lord your God, failing to observe his commands, his laws and his decrees that I am giving you this day.12 Otherwise, when you eat and are satisfied, when you build fine houses and settle down, 13 and when your herds and flocks grow large and your silver and gold increase and all you have is multiplied, 14 then your heart will become proud and you will forget the Lord your God, who brought you out of Egypt, out of the land of slavery. 15 He led you through the vast and dreadful wilderness, that thirsty and waterless land, with its venomous snakes and scorpions. He brought you water out of hard rock.16 He gave you manna to eat in the wilderness, something your ancestors had never known, to humble and test you so that in the end it might go well with you. 17 You may say to yourself, “My power and the strength of my hands have produced this wealth for me.” 18 But remember the Lord your God, for it is he who gives you the ability to produce wealth, and so confirms his covenant, which he swore to your ancestors, as it is today.
19 If you ever forget the Lord your God and follow other gods and worship and bow down to them, I testify against you today that you will surely be destroyed. 20 Like the nations the Lord destroyed before you, so you will be destroyed for not obeying the Lord your God.

God reminds the Israeli people of His goodness to them.  God  rescued them from slavery in Egypt . Then God lead them safely through the dessert and provided food and water for them. God wants the people to be thankful to Him and appreciate His goodness. They should not think that their success is due to their own abilities and efforts.
Let us always be thankful to God for His goodness and for all His blessings to us. Let us look back over our lives and see God’s hand and how He has blessed us. 


JUMATATU TAREHE 19 AGOSTI 2019 ASUBUHI      
KUMBUKUMBU LA TORATI 8:11-20
11 Jihadhari, usije ukamsahau Bwana, Mungu wako, kwa kutozishika amri zake, na hukumu zake, na sheria zake, ninazokuamuru leo. 
12 Angalia, utakapokuwa umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake; 
13 na makundi yako ya ng'ombe na kondoo yatakapoongezeka, na fedha yako na dhahabu yako itakapoongezeka, na kila kitu ulicho nacho kitakapoongezeka; 
14 basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahau Bwana, Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa; 
15 aliyekuongoza katika jangwa lile kubwa lenye kitisho, lenye nyoka za moto na nge, nchi ya kiu isiyokuwa na maji; aliyekutolea maji katika mwamba mgumu, 
16 aliyekulisha jangwani kwa mana, wasiyoijua baba zako; apate kukutweza, apate kukujaribu, ili kukutendea mema mwisho wako. 
17 Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo. 
18 Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo. 
19 Lakini itakuwa, kama ukimsahau Bwana, Mungu wako, na kuiandama miungu mingine, na kuitumikia na kuiabudu, nawashuhudia leo ya kuwa mtaangamia bila shaka. 
20 Kama vile mataifa yale ambayo Bwana anawaangamiza mbele yenu, ndivyo mtakavyoangamia; kwa sababu hamkutaka kuisikiliza sauti ya Bwana, Mungu wenu.

 Mungu aliwakumbusha Waisraeli kuhusu matendo makuu mema ambaye aliwatendea. Mungu aliwaokoa Waisraeli kutoka utumwani kule Misri. Aliwaongoza kupita jangwani na kuwalindi na kuwapa chakula na maji. Mungu alitaka watu kukiri msaada wa Mungu na kutufikiri  kwamba mafanyikio wao ni kwa uwezo wao tu.
Mungu anataka shukurani zetu kwa matendo yake makuu katika maisha yetu. Tutafakari kuhusu maisha yetu na tuangalia matendo makuu ya baraka ambao Mungu ametutendea. Tuwe na shukrani.