Date: 
30-07-2020
Reading: 
Deuteronomy 32:1-7

THURSDAY 30TH JULY 2020   MORNING                                                 

Deuteronomy 32:1-7 New International Version (NIV)

1 Listen, you heavens, and I will speak
    hear, you earth, the words of my mouth.
Let my teaching fall like rain
    and my words descend like dew,
like showers on new grass,
    like abundant rain on tender plants.

I will proclaim the name of the Lord.
    Oh, praise the greatness of our God!
He is the Rock, his works are perfect,
    and all his ways are just.
A faithful God who does no wrong,
    upright and just is he.

They are corrupt and not his children;
    to their shame they are a warped and crooked generation.
Is this the way you repay the Lord,
    you foolish and unwise people?
Is he not your Father, your Creator,[a]
    who made you and formed you?

Remember the days of old;
    consider the generations long past.
Ask your father and he will tell you,
    your elders, and they will explain to you.

Everyone should realize that, our existence is because of God. He created us and purchased us back from the bondage of sin. Under his protection, we may find refuge from all our enemies, and in all our troubles. 


ALHAMISI TAREHE 30 JULAI 2020   ASUBUHI                                        

KUMBUKUMBU 32:1-7

1 Sikilizeni, enyi mbingu, nami nitanena; Na nchi isikie maneno ya kinywa changu.
Mafundisho yangu yatadondoka kama mvua, Maneno yangu yatatona-tona kama umande; Kama manyunyu juu ya majani mabichi; Kama matone ya mvua juu ya mimea.
Maana nitalitangaza Jina la Bwana; Mpeni ukuu Mungu wetu.
Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili.
Wametenda mambo ya uharibifu, Hawawi watoto wake, hii ndiyo ila yao; Wao ni kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka.
Je! Mnamlipa Bwana hivi, Enyi watu wapumbavu na ujinga? Je! Yeye siye baba yako aliyekununua? Amekufanya, na kukuweka imara.
Kumbuka siku za kale, Tafakari miaka ya vizazi vingi; Mwulize baba yako, naye atakuonyesha; Wazee wako, nao watakuambia.

Ni vyema kila mtu akatambua kuwa, kuishi kwetu ni kwa sababu ya Mungu. Yeye alituumba na kutununua kutoka katika utumwa wa dhambi. Tukiwa chini ya ulinzi wake, tunapata kimbilio dhidi ya maadui zetu, na anatukingia shida zetu zote.