Date: 
17-09-2018
Reading: 
Colossians 2:16-23 (Wakolosai 2:16-23)

MONDAY 17TH SEPTEMBER 2018 MORNING                            

Colossians 2:16-23 New International Version (NIV)

Freedom From Human Rules

16 Therefore do not let anyone judge you by what you eat or drink, or with regard to a religious festival, a New Moon celebration or a Sabbath day. 17 These are a shadow of the things that were to come; the reality, however, is found in Christ. 18 Do not let anyone who delights in false humility and the worship of angels disqualify you. Such a person also goes into great detail about what they have seen; they are puffed up with idle notions by their unspiritual mind. 19 They have lost connection with the head, from whom the whole body, supported and held together by its ligaments and sinews, grows as God causes it to grow.

20 Since you died with Christ to the elemental spiritual forces of this world, why, as though you still belonged to the world, do you submit to its rules: 21 “Do not handle! Do not taste! Do not touch!”? 22 These rules, which have to do with things that are all destined to perish with use, are based on merely human commands and teachings. 23 Such regulations indeed have an appearance of wisdom, with their self-imposed worship, their false humility and their harsh treatment of the body, but they lack any value in restraining sensual indulgence.

This week we are thinking about Christian Freedom. Christianity is not a religion of rules and regulations. We can not make ourselves righteous and acceptable to God by following a set of rules or rituals. We are saved by Grace through faith in Jesus Christ who died for us. We need to live

Our lives lead by the Holy Spirit. Pray that God would change you from inside so that you are pure in thought and word and deed. 

JUMATATU TAREHE 17 SEPTEMBA 2018 ASUBUHI                 

KOLOSAI  2:16-23

16 Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; 
17 mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo. 
18 Mtu asiwanyang'anye thawabu yenu, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kuabudu malaika, akijitia katika maono yake na kujivuna bure, kwa akili zake za kimwili; 
19 wala hakishiki Kichwa, ambacho kwa yeye mwili wote ukiruzukiwa na kuungamanishwa kwa viungo na mishipa, hukua kwa maongeo yatokayo kwa Mungu. 
20 Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani, 
21 Msishike, msionje, msiguse; 
22 (mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu? 
23 Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili.

Wiki hii tunatafakari kuhusu Uhuru wa Mkristo. Ukristo siyo dini ya sheria. Hatuwezi kuokolewa kwa nguvu zetu. Hatuwezi kupata haki mbele ya Mungu kwa njia ya kufuata sheria na utaratibu za kidini. Tunaokolewa kwa neema kwa njia ya Imani. Tunatubu dhambi zetu na kumwamini Yesu Kristo ambaye ametufia msalabani. Tunapaswa kuishi tukiongozwa na Roho Mtakatifu. Tumwombe Mungu atutakase kutoka moyoni ili mawazo, maneno na matendo yetu yawe safi.