Event Date: 
02-08-2021

Katika kuhakikisha injili inafika kwa walengwa na kwa wakati, Baraza la Wazee la Usharika wa Kanisa Kuu Azaniafront Cathedral, siku ya Ijumaa, tarehe 30/07/2021 lilikabidhi pikipiki mpya aina ya Honda kwa Mch. Mmbuji anayesimamia eneo linalomilikiwa na Azaniafront la Kiharaka wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.

Pikipiki hiyo imenunuliwa kwa michango ya Wazee wa Bazara wa Azaniafront na ilikabidhiwa na Ndg Cuthbert Swai aliyeambatana na Ndg Doris Maro, ambao wote ni wajumbe wa Baraza hilo.

Pikipiki hiyo itamsaidia Mch. Mmbuji katika shughuli zake za kila siku katika kulihudumia eneo hilo ambapo mradi wa ujenzi wa Kituo cha Kiroho cha Kiharaka unaendelea.

---------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

PICHA: Ndg Cuthbert Swai pamoja na Ndg Doris Maro katika matukio tofauti wakati wakikabidhi pikipiki mpya aina ya Honda kwa Mchungaji Mmbuji wa eneo la Kiharaka.

                                                                                        ####