Date: 
06-11-2021
Reading: 
Ayubu 22:21-22

Jumamosi asubuhi tarehe 06.11.2021

Ayubu 22:21-22

21 Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; 
Ndivyo mema yatakavyokujia.
22 Uyapokee, tafadhali, mafunzo yatokayo kinywani mwake, 
Na maneno yake yaweke moyoni mwako.

Mwenye haki ataishi kwa imani;

Katika sura ya 22, Elifazi Mtemani anaelezea uovu wa Ayubu! Anahoji ukamilifu wa Ayubu mbele za Mungu! Anauliza kuwa anamfaa Mungu? 

Tafakari hii ni fupi, sitakwenda kwenye historia kuchambua ilikuwaje hadi akasema hivyo, kwa nini? Alimaanisha nini? Na matokeo yake ilikuwa nini. 

Tuangalie ujumbe wake baadala ya tuhuma kwa Ayubu. Kwamba tumjue sana Mungu ili tuwe na amani ndipo mema yatatujia, tukiyapokea mafunzo yatokayo kinywani mwake na kuyahifadhi mioyoni mwetu.

Tunaitwa kuwa na Yesu, ili amani ya Mungu ikae nasi, tukilisoma neno la Mungu lituongoze maishani. Ukomavu wa imani yetu unategemea neno la Mungu katika maisha yetu.

Jumamosi njema.