Date: 
10-03-2022
Reading: 
Amosi 7:1-9

Hii ni Kwaresma 

Alhamisi asubuhi tarehe 10.02.2022

Amosi 7:1-6

1 Haya ndiyo aliyonionyesha Bwana MUNGU; tazama, aliumba nzige mwanzo wa kuchipuka kwake mimea wakati wa vuli; na tazama, ilikuwa mimea ya wakati wa vuli baada ya mavuno ya mfalme.

2 Ikawa, nzige walipokwisha kula majani ya nchi, ndipo nikasema, Ee Bwana MUNGU, samehe, nakusihi; Yakobo atasimamaje? Kwa maana ni mdogo.

3 Bwana akaghairi katika jambo hili. Jambo hili halitakuwa, asema Bwana.

4 Haya ndiyo aliyonionyesha Bwana MUNGU; tazama, Bwana MUNGU aliita ili kushindana kwa moto; nao ukavila vilindi vikuu, ukataka kuiteketeza nchi kavu.

5 Ndipo nikasema, Ee Bwana MUNGU, acha, nakusihi; Yakobo atasimamaje? Kwa maana ni mdogo.

6 Bwana akaghairi katika jambo hili pia. Jambo hili halitakuwa, asema Bwana MUNGU.

Tukimtegemea Bwana Tutashinda majaribu;

Amosi anaandika juu ya ukuu wa Mungu, lakini pia akionesha kuwa Mungu ni wa haki. Mungu anaonesha hasira yake kwa Israeli kwa kutuma nzige waliokula mimea yote, lakini anasamehe kwa kumsikiliza Amosi. Amosi anaomba msamaha kwa niaba ya Israeli.

Hasira ya Mungu ipo pale tusipomsikia na kumtii. Mungu ni wa haki, atatuhukumu kwa kadri ya matendo yetu. Majaribu hutufanya tumkosee Mungu, na kutupeleka hukumuni. Kumbe tufanye nini?

Tukimtegemea Bwana Tutashinda majaribu.

Siku njema.