Date: 
01-02-2021
Reading: 
ACTS 8:18-25 Matendo 8:18-25

MONDAY 1ST  FEBRUARY 2021    MORNING                                              

ACTS 8:18-25 New International Version (NIV)

18 When Simon saw that the Spirit was given at the laying on of the apostles’ hands, he offered them money 19 and said, “Give me also this ability so that everyone on whom I lay my hands may receive the Holy Spirit.”

20 Peter answered: “May your money perish with you, because you thought you could buy the gift of God with money! 21 You have no part or share in this ministry, because your heart is not right before God. 22 Repent of this wickedness and pray to the Lord in the hope that he may forgive you for having such a thought in your heart. 23 For I see that you are full of bitterness and captive to sin.”

24 Then Simon answered, “Pray to the Lord for me so that nothing you have said may happen to me.”

25 After they had further proclaimed the word of the Lord and testified about Jesus, Peter and John returned to Jerusalem, preaching the gospel in many Samaritan villages.

This passage reminds all Christians to re-evaluate our commitment to Jesus Christ. 

It is not seeing a miracle or believing in the miracle that saves but only the power of Christ alone saves.

     


                                                                                                                                                              

JUMATATU TAREHE 1 FEBRUARI 2021     ASUBUHI                             

MATENDO 8:18-25

18 Hata Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha akisema,
19 Nipeni na mimi uwezo huu, ili kila mtu nitakayemweka mikono yangu, apokee Roho Mtakatifu.
20 Lakini Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali.
21 Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu.
22 Basi, tubia uovu wako huu, ukamwombe Bwana, ili kama yamkini, usamehewe fikira hii ya moyo wako.
23 Kwa maana nakuona u katika uchungu kama nyongo, na tena u katika kifungo cha uovu.
24 Simoni akajibu, akasema, Niombeeni ninyi kwa Bwana, yasinifikilie mambo haya mliyosema hata moja.
25 Nao walipokwisha kushuhudia na kulihubiri neno la Bwana wakarudi Yerusalemu, wakaihubiri Injili katika vijiji vingi vya Wasamaria.

Kifungu hiki kinatukumbusha Wakristo wote kutathmini tena ufuasi wetu kwa Yesu Kristo.

Wokovu  haupatikani kwa kuona au kuamini katika miujiza, bali nguvu ya Yesu Kristo pekee ndiyo inayotuokoa.