Date: 
24-07-2020
Reading: 
Acts 20:7-12 (Matendo 20:7-12)

FRIDAY 24TH JULY 2020 MORNING                                                       

Acts 20:7-12 New International Version (NIV)

On the first day of the week we came together to break bread. Paul spoke to the people and, because he intended to leave the next day, kept on talking until midnight. There were many lamps in the upstairs room where we were meeting. Seated in a window was a young man named Eutychus, who was sinking into a deep sleep as Paul talked on and on. When he was sound asleep, he fell to the ground from the third story and was picked up dead. 10 Paul went down, threw himself on the young man and put his arms around him. “Don’t be alarmed,” he said. “He’s alive!” 11 Then he went upstairs again and broke bread and ate. After talking until daylight, he left. 12 The people took the young man home alive and were greatly comforted.

God did not punish Eutichus for sleeping during the service, He valued Eutychus' life and passion to have fellowship and break bread with his fellow believers, even as it was beyond his bedtime. The young man died, but He brought Eutychus back to life through the hands of Paul.

God cares about every single thing that we do for Him. 1 Corinthians 15:58 tells us,

"Therefore, my beloved brethren, be steadfast, immovable, always abounding in the work of the Lord, knowing that your labor is not in vain in the Lord."


IJUMAA TAREHE 24 JULAI 2020  ASUBUHI                           

MATENDO YA MITUME  20:7-12

Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane.
Palikuwa na taa nyingi katika orofa ile tulipokuwa tumekusanyika.
Kijana mmoja, jina lake Eutiko, alikuwa ameketi dirishani, akalemewa na usingizi sana; hata Paulo alipoendelea sana kuhubiri, akazidiwa na usingizi wake akaanguka toka orofa ya tatu; akainuliwa amekwisha kufa.
10 Paulo akashuka, akamwangukia, akamkumbatia, akasema, Msifanye ghasia, maana uzima wake ungalimo ndani yake.
11 Akapanda juu tena, akamega mkate, akala, akazidi kuongea nao hata alfajiri, ndipo akaenda zake.
12 Wakamleta yule kijana, yu mzima, wakafarijika faraja kubwa sana.

Mungu hakumuadhibu Eutiko kwa sababu alilala wakati wa ibada, alithamini maisha yake na shauku aliyokuwa nayo ya kuwa na ushirika na wenzake pamoja na kushiriki Chakula cha Bwana pamoja na waumini wenzake; pamoja na kwamba muda wake wa kulala ulikwishapita. Kijana huyu alifariki, lakini Mungu alimfufua kupitia mikono ya Paulo.

Mungu anajali kila jambo tufanyalo kwa ajili yake.  1 Wakorintho 15:58 inatueleza,

" Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana."