Date: 
28-09-2018
Reading: 
Acts 1:21-26 (Matendo 1:21-26)

FRIDAY 28TH SEPTEMBER 2018 MORNING                                

Acts 1:21-26 New International Version (NIV)

21 Therefore it is necessary to choose one of the men who have been with us the whole time the Lord Jesus was living among us, 22 beginning from John’s baptism to the time when Jesus was taken up from us. For one of these must become a witness with us of his resurrection.”

23 So they nominated two men: Joseph called Barsabbas (also known as Justus) and Matthias. 24 Then they prayed, “Lord, you know everyone’s heart. Show us which of these two you have chosen 25 to take over this apostolic ministry, which Judas left to go where he belongs.” 26 Then they cast lots, and the lot fell to Matthias; so he was added to the eleven apostles.

The remaining 11 Apostles realized that it was important to replace  Judas Iscariot. The apostles wanted to be sure to choose the right person according to God’s will. They thought about what type of person to choose and proposed two names and then they prayed  asking for God’s guidance. Then they cast lots trusting that the right person would be chosen.

Let us follow their example and pray for God’s guidance before we make any important decisions.       

IJUMAA TAREHE 28 SEPTEMBA 2018 ASUBUHI                                

MATENDO 1:21-26

21 Basi katika watu waliofuatana nasi wakati wote Bwana Yesu alipokuwa akiingia na kutoka kwetu, 
22 kuanza tangu ubatizo wa Yohana, hata siku ile alipochukuliwa kwetu kwenda juu, inapasa mmoja wao awe shahidi wa kufufuka kwake pamoja nasi. 
23 Wakaweka wawili, Yusufu, aitwaye Barsaba, aliyekuwa na jina la pili Yusto, na Mathiya. 
24 Kisha wakaomba, wakasema, Wewe, Bwana, ujuaye mioyo ya watu wote, tuonyeshe ni nani uliyemchagua katika hawa wawili, 
25 ashike mahali katika huduma hii na utume huu, alioukosa Yuda, aende zake mahali pake mwenyewe. 
26 Wakawapigia kura; kura ikamwangukia Mathiya; naye akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmoja.

Baada Yuda Iskariote kuondoka wale Mitume 11 walijua ni muhimu kumchagua mtume mwingine badala ya Yuda. Walitafakari kuhusu sifa ya mhusika na kupendekeza majina mawili. Halafu walimwomba Mungu awaongoze katika uchaguzi.

Tufuate mfano wao. Tumwombe Mungu atuongoze kabla ya kufanya maamuzi yoyote muhimu.