Date: 
18-08-2021
Reading: 
2 Wakorintho 11:7-15 (Corinthians)

JUMATANO TAREHE 18/08/2021, ASUBUHI.

2 Wakorintho 11:7-15

Je! Nalifanya dhambi kwa kunyenyekea ili ninyi mtukuzwe, kwa sababu naliwahubiri Injili ya Mungu bila ujira?
Naliwanyang'anya makanisa mengine mali yao, nikitwaa posho langu ili niwahudumie ninyi.
Nami nilipokuwa pamoja nanyi na kuhitaji sikumlemea mtu. Maana hao ndugu waliokuja kutoka Makedonia walinipa kadiri ya mahitaji yangu; nami katika mambo yote najilinda nafsi yangu nisiwalemee hata kidogo; tena najilinda.
10 Kama vile ile kweli ya Kristo ilivyo ndani yangu, hakuna mtu atakayenifumba kinywa katika kujisifu huku, katika mipaka ya Akaya.
11 Kwa nini? Je! Ni kwa sababu siwapendi ninyi? Mungu anajua.
12 Lakini nifanyalo nitalifanya, ili niwapinge hao watafutao nafasi wasipate nafasi; ili kwamba katika neno hilo wajisifialo waonekane kuwa kama sisi.
13 Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo.
14 Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.
15 Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.

Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema;

Mtume Paulo anawaonya mitume wafanyao kazi yao kwa uongo waache mara moja. Anawaasa wasifanye kazi kwa hila. Anawafananisha na shetani ajigeuzaye malaika wa nuru. Anawasihi kuwa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.

Nini tabia yetu katika maisha na kazi zetu kwa ujumla? Tu wakweli na waadilifu? Tuache maisha ya uongo na ujanja ujanja, yaliyojaa hila. Tuishi kwa uhalisia.

Uchaji na utii wa neno la Mungu ndio maisha yanayofaa, bila kusahau unyenyekevu mbele za Mungu. Tufahamu kuwa mwisho wetu utategemea kazi zetu hapa duniani.

Siku njema.


WEDNESDAY 18TH AUGUST 2021, MORNING

2 CORINTHIANS 11:7-15 (NIV)

Was it a sin for me to lower myself in order to elevate you by preaching the gospel of God to you free of charge? I robbed other churches by receiving support from them so as to serve you. And when I was with you and needed something, I was not a burden to anyone, for the brothers who came from Macedonia supplied what I needed. I have kept myself from being a burden to you in any way, and will continue to do so. 10 As surely as the truth of Christ is in me, nobody in the regions of Achaia will stop this boasting of mine. 11 Why? Because I do not love you? God knows I do!

12 And I will keep on doing what I am doing in order to cut the ground from under those who want an opportunity to be considered equal with us in the things they boast about. 13 For such people are false apostles, deceitful workers, masquerading as apostles of Christ. 14 And no wonder, for Satan himself masquerades as an angel of light. 15 It is not surprising, then, if his servants also masquerade as servants of righteousness. Their end will be what their actions deserve.

Read full chapter

God opposes the proud, but gives grace to the humble;

The apostle Paul warns the apostles who are falsely at work to stop immediately. He urges them not to work subtly. He likens them to a devil who disguises himself as an angel of light. He urges them to be ministers of righteousness, whose end will be according to their works.

What is our attitude in life and our work in general? Are we honest and upright? Let us leave a life of lies and cunning, full of deceit. Let us live in reality.

Reverence and obedience to God's word are the best way of life, not to mention humility before God. We know that our end will depend on our work here on earth.

Good day.