Date: 
18-03-2022
Reading: 
2 Samweli 13:16

Ijumaa asubuhi tarehe 18.03.2022

2 Samweli 13:16

Naye akamwambia, Sivyo, kwa kuwa mabaya haya ya kunitoa ni makuu kuliko yale uliyonitendea. Lakini alikataa kumsikiliza.

Tupinge ukatili;

Amnoni alimtamani ndugu yake Tamari, akajifanya mgonjwa. Tamari akatumwa na Daudi akampikie ndugu yake mgonjwa, Amnoni. Amnoni akatumia fursa hiyo kumbaka Tamari.

Baada ya kumbaka, Amnoni alimchukia Tamari kuliko alivyompenda mwanzo. Akamfukuza. Ndipo sasa somo la asubuhi hii ni Tamari akimjibu Amnoni alipokuwa akimfukuza; Soma tena;

2 Samweli 13:16 Naye akamwambia, Sivyo, kwa kuwa mabaya haya ya kunitoa ni makuu kuliko yale uliyonitendea. Lakini alikataa kumsikiliza.

Amnoni alimfanyia Tamari ukatili, alimbaka. Hakuishia hapo, anamfukuza. Ukisoma zaidi unaona Tamari akimwambia Amnoni kuwa anafanya jambo la kipumbavu.

Matumizi ya nguvu, mamlaka na uonevu siyo jambo jema, huumiza watu wasio na hatia. Siyo kusudi la Mungu watu wateseke duniani, hivyo tunapowaonea wenzetu tunamkosea Mungu.

Siku njema.