Date: 
17-11-2020
Reading: 
2 Peter 3:1-7

TUESDAY 17TH NOVEMBER 2020   MORNING                                                      

2 Peter 3:1-7 New International Version (NIV)

Dear friends, this is now my second letter to you. I have written both of them as reminders to stimulate you to wholesome thinking. I want you to recall the words spoken in the past by the holy prophets and the command given by our Lord and Savior through your apostles.

Above all, you must understand that in the last days scoffers will come, scoffing and following their own evil desires. They will say, “Where is this ‘coming’ he promised? Ever since our ancestors died, everything goes on as it has since the beginning of creation.” But they deliberately forget that long ago by God’s word the heavens came into being and the earth was formed out of water and by water. By these waters also the world of that time was deluged and destroyed. By the same word the present heavens and earth are reserved for fire, being kept for the day of judgment and destruction of the ungodly.

God’s Word clearly says that God created the world by His word, judged the world at the flood by His word, and will judge the ungodly when Christ returns by His word. Therefore we must stand firm on these truths and out of love warn everyone to flee the wrath to come.


JUMANNE TAREHE 17 NOVEMBA 2020  ASUBUHI                                              

2 PETRO 3:1-7

1 Wapenzi, waraka huu ndio wa pili niwaandikiao ninyi; katika zote mbili naziamsha nia zenu safi kwa kuwakumbusha,
2 mpate kuyakumbuka yale maneno yaliyonenwa zamani na manabii watakatifu, na ile amri ya Bwana na Mwokozi iliyoletwa na mitume wenu.
3 Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe,
4 na kusema, Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa.
5 Maana hufumba macho yao wasione neno hili ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia, imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la Mungu;
6 kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia.
7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.

Neno la Mungu linasema wazi kuwa Mungu aliumba dunia kwa Neno lake, na kwa Neno lake aliihukumu dunia kwa gharika, na kwa Neno lake atawahukumu wasio haki Kristo atakaporudi. Hivyo basi, ni lazima tusimame katika kweli hii; na kwa njia ya upendo tuwaonye watu wote wapate kuikimbia hasira hii inayokuja.