Date: 
26-01-2022
Reading: 
1Yohana 1:1-4

Jumatano asubuhi tarehe 26.01.2022

1 Yohana 1:1-4

1 Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima;

2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);

3 hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.

4 Na haya twayaandika, ili furaha yetu itimizwe.

Mungu anaondoa ubaguzi;

Yohana anaanza kuandika waraka wake kwa kusisitiza Neno la uzima lililokuwepo, lililopo na litakalokuwepo. Yohana anaonesha kutengeneza ushirika wa Kikristo kwa njia ya kuhubiri neno la Mungu. Anahimiza umoja kwa njia ya imani, katika neno la Mungu.

Yohana anatukumbusha kudumu katika umoja, kama taifa la Mungu, kwa njia ya neno lake. Ukiendelea kusoma mistari inayofuata, Yohana anatuhimiza kukaa pamoja kwa kukumbushana yatupasayo katika kazi zetu, tukiwa watu wa toba. Yesu anatuita kuondoa ubaguzi kwa kukaa pamoja kama Taifa lake.

Jumatano njema.